Sambaza:

Ni mwaka mmoja ila inaonekana kama jana tangu TECNO Mobile walivyotoa simu iliyoongoza kwenye sekta ya smartphone – Phantom 6 & Phantom 6 Plus ambayo ilianzisha mfumo wa kamera mbili nyuma, vipengele/sifa za kipekee na mtindo mwembamba uliotengenezwa Dubai. Phantom 6 ilikuwa moja ya mambo mazuri yaliyotokea katika soko la smartphone mwezi Septemba 2016  ilipozinduliwa huko Burj Khalifa, Dubai.

Mwaka huu, wachambuzi wa simu za mkononi na vyombo vya habari kwa ujumla wameweka jicho la karibu kwenye brand hiyo ya simu za mkononi ili kupata maelezo ya kwanza kuhusu toleo jipya la Phantom – eneo la uzinduzi, model name, bei na muundo muhimu zaidi wa bidhaa. Kukiwa na picha mpya za Phantom zinazosambaa mtandaoni, ni salama kusema kwamba hatimaye tuna taarifa kuhusu kifaa kinachotarajia.

Kamera za nyuma mbili zilizounganishwa kwenye simu mpya ya Tecno Phantom

Toleo jipya la Phantom ni jembamba sana na inaendelea kupeperusha bendera ya muundo wa kisasa kama watangulizi wake. Kamera zake mbili za nyuma  zimewekewa mtindo mpya kabisa na zimewekwa sambamba upande wa kushoto wa simu. Kamera hazijavimba na zinavutia, kifaa hicho kimefungwa na chuma kwa nje.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno L9 Plus bei na Sifa zake
Phantom

Neno Phantom 8 – linatosha kuthibitisha jina la Phantom inayofuata? Pengine

Ndio, picha zilizotolewa zinaeleza mengi kuhusu kukamilika kwa kifaa cha kifahari na watumiaji wanaachwa na maswali tu na kufikiria ni zipi specs za ndani za kifaa hiki, usafi wake, swag, utendaji na bei zitakuwaje; Sidhani kama tunatakiwa kusubiri kwa muda mrefu kwa sababu uzinduzi unaonekana upo kwenye kona.

Umeipenda makala hii ? Tuandikie kupitia sehemu yetu ya maoni, pia usisahau kuandika barua pepe yako ili tukutumie taarifa kila tunavyozipandisha.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako