Tecno Phantom 5

Tecno Mobile, mwaka wa 2015 ilileta smartphone nzuri yenye 4G iliyoitwa Tecno Phantom 5. Upande wa pili Huawei baada ya kuizindua Huawei P8, waliamua kuleta toleo nyingine la simu hiyo, hii ni Huawei P8 Lite. Zina utofauti katika ukubwa wa kuhifadhi vitu na uwezo wa kufanya kazi muda mrefu.

Leo natumia muda wangu kulinganisha Tecno Phantom 5 vs Huawei P8 Lite baada ya moja ya wafuatiliaji wa mediahuru kuniuliza ipi ni kali zaidi. Naam nadhani hii itakupa mtazamo bora na kulinganisha simu hizi mbili Tecno Phantom 5 vs Huawei P8 Lite. Simu janja zote ni nzuri na zinatumia moja ya mfumo wa kisasa wa uendeshaji ambao ni Android Lollipop.

Hebu tuziangalie kiundani simu hizi baada ya kukupa maelezo mafupi ya nini nitakacho kizungumzia.

Kuonyesha Vizuri

Tecno Phantom 5 ina kioo kizuri kuliko mwenzake, Huawei P8 Lite. Kwa nini nasema hivyo?

Tecno Phantom 5 ina kioo chenye inchi 5.5 HD, uwezo wa skrini wa 1080 x 1920 pixels na uwiano wa pixel wa 400ppi.

SOMA NA HII:  Ishara 7 ambazo zinaonyesha huwezi kuishi bila ya simu ya mkononi

Hiyo ni bora, ukinganisha na kioo cha inchi 5.0 cha Huawei P8 Lite ikiwa na uwezo wa pixels 720 x 1280 na 294ppi.

Uwezo wa Mfumo wa Uendeshaji

Naam, awali nilisema simu janja zote mbili zinatumia OS ya Android 5.0 Lollipop. Hata hivyo, toleo la OS hizi zinatofautiana kwenye simu zote mbili.

Tecno Phantom 5 inaendeshwa na Android 5.1.1 Lollipop ya hivi karibuni. Wakati Huawei P8 Lite inaendeshwa kwenye mfumo wa Android 5.0.2 Lollipop. Unaweza kuona utofauti. Phantom 5 ina UI bora zaidi kuliko Huawei P8 Lite na utendaji mzuri zaidi kwa sababu inatumia sasisho au toleo lililoboreshwa la OS ya P8 Lite.

Uwezo wa Prosesa na RAM

Ipi kati ya hizi mbili inatumia prosesa bora na yenye nguvu? Kura yangu naipa Tecno Phantom 5. Kwa nini?

Tecno Phantom 5 inawezeshwa na octa-core (8-cores) Cortex A7 processor ikiwa na kiwango cha 1.5GHz hiyo ndio nguvu ninayoisema mimi.

SOMA NA HII:  Simu 9 Bora za Tecno unazoweza kununua 2017 - Uwezo na Bei

Hebu tuangalie kile tunachokipata kwenye Huawei P8 Lite. Inatumia octa-core processor inayofanya mzunguko kwa kiwango cha 1.2GHz.

Kwa upande wa Primary Memory (RAM), Tecno Phantom 5 inachukua kura zote tena. Ina 3GB (3072MB) ya RAM, pamoja na 1.5GHz na octa-core processor, unakuwa na uhakika na simu yako.

Huawei P8 Lite kwa upande mwingine ina 2GB (2048MB) ambayo pia inafanya kazi vizuri na kwa ufanisi ikiwa na processor yenye 1.2GHz.

Tecno Phantom 5 inashida tena kwa 3GB ya RAM.

Kumbukumbu na Uhifadhi

Uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu ni bora zaidi. Je ni simu gani ina uwezo mkubwa wa uhifadhi ? ROM ni hifadhi ya ndani ya simu, bila kadi ya MicroSD.

Tecno Phantom 5 ina hifadhi ya ndani ya 32GB. Hata hivyo, huwezi kuweka kadi ya MicroSD.
Huawei P8 upande wa pili ina 26GB ya ROM.

SOMA NA HII:  Bei mpya za simu za tecno nchini Tanzania

Uwezo wa Upanuzi
Tecno Phantom 5 haina sehemu ya kuweka kadi ya MicroSD. Hii ina maana kwamba inategemea uhifadhi wa ndani wa 32GB.

Huawei P8 ina uwezo wa kuongezwa uhifadhi kwa sababu ina MicroSD card slot, unaweza kuweka memori hadi 128GB.

Ulinganisho wa kamera

Kamera ya Nyuma (Kamera ya Msingi)

Tecno Phantom 5 ina kamera ya nyuma ya 13.0MP. Pia ina LED flash ambayo inakuhakikishia kupiga picha zenye ubora wakati wa mwanga mdogo.

Huawei P8 Lite pia ina kamera ya msingi ya 13.0MP. Ambayo pia ina LED flash.

Kamera ya mbele (Kamera ya Selfie)
Tecno Phantom 5 ina shooter ya mbele ya 8.0MP bora kuliko Huawei P8 Lite ambayo ina kamera ya mbele ya 5.0MP.

Uwezo wa Betri

Tecno Phantom 5 inatumia betri yenye nguvu ya 3000mAh lithiamu-ion. Kwa upande mwingine Huawei P8 ina 2200mAh. Hii inamaanisha kwamba Tecno Phantom 5 itafanya kazi muda mrefu zaidi kuliko Huawei P8 Lite./em

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako