Habari za Teknolojia

Fahamu dili walioingia Tecno Mobile na klabu ya Manchester city

on

Watengezaji wakubwa wa simu za mkononi TECNO Mobile na Klabu ya ligi ya Uingereza, Manchester City wamesherehekea uzinduzi wa ushirikiano wa kimataifa kwa miaka kadha kama mshirika rasmi wa Klabu ya mpira ya Manchester City. TECNO Mobile itashirikiana na klabu hiyo kukuza mikakati ya masoko na matangazo ya kampeni sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo bara la Afrika ambapo TECNO tayari inatambulika kama kinara wa soko la simu za mkononi.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa ushirikiano huo wa kimataifa uliofanyika kwenye kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya vijana, Afisa Mkuu wa Biashara wa City Football Group Tom Glick amesema

“Tunafurahi kuwakaribisha TECNO Mobile katika mkusanyiko wa ushirikiano wa kimataifa, kujikita kwake zaidi katika masoko ya nyumbani kunaendana na namna ambavyo tunafanya shughuli zetu na tunatazamia kushirikiana nao kuungana na mashabiki wa Manchester City duniani kote”

Vile vile Mkurugenzi Mtendaji wa TECNO Mobile Stephen Ha alizungumza katika uzinduzi huo wa kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya vijana cha Manchester City kwamba

“Tunashukuru sana kushirikiana na klabu yenye mafanikio na inayojulikana ya Manchester City, tutaendeleza uhusiano wetu wa muda mrefu katika michezo kwa hali ya juu kwa kuwapatia wateja wetu uzoefu wakufurahia zaidi simu bora isiyolinganishwa na nyingine”

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.