Tecno Mobile ni kampuni ya simu za mkononi inayomilikiwa na kampuni ya Transsion Holdings ambayo makao yake makuu yapo nchini Hong Kong – China, kampuni hii ilianzishwa Julai 2006.

Tecno Mobile

Pamoja na kituo chake cha kwanza cha utafiti na maendeleo jijini Shanghai, China, Tecno Mobile ilianzishwa kama Tecno Telecom Limited kulenga utafiti na maendeleo ya simu za mkononi na bidhaa zake., lakini baadaye ikabadilisha jina lake kuwa Transsion Holdings na Tecno Mobile inafanya kazi kama moja ya matawi yake.

Mwaka 2007 Tecno ilianzisha kampui nyingine ya simu nchini India kwa jina la Itel ambayo Mei 2017 ilitambuliwa kama “bidhaa rafiki zaidi kwa wanafunzi“.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuflash Simu za Tecno kwa Urahisi

Hata hivyo, baada ya utafiti wa soko uliofanywa Asia ya Kusini-Mashariki, Afrika na Latin America, kampuni hiyo iligundua kwamba Afrika ilikuwa eneo lenye faida zaidi. Matokeo yake, mwaka wa 2008, ilisimamisha biashara zake barani Asia ili kuzingatia Afrika tu . Mwaka wa 2010 iliingia kwenye kampuni tatu za simu za mkononi maarufu zaidi barani Afrika.

Mwaka 2012, Tecno ilitoa simu janja ya kwanza iliyotengenezwa Ethiopia.  Tecno ilitangaza simu yake ya kwanza  kutumia mfumo wa uendeshaji wa Marshmallow mwaka 2016 .

Mwaka wa 2016, Tecno Mobile ilizindua “Smartphone zenye kamera nzuri barani Afrika”. Katika mwaka huo huo, Tecno ilizindua Tecno Phantom 6 na Tecno Phantom 6 Plus na usalama wa uthibitishaji wa Biometri.

SOMA NA HII:  Kuweka Mkeka "Kubeti" Njia ya Kutengeneza Pesa yenye Ugonjwa

Baadaye mwaka wa 2016, Tecno iliingia kwenye soko la Mashariki ya kati baada ya kupata soko zuri Afrika, na kisha katika Asia ya Kusini mashariki. Mwaka wa 2017, Tecno Mobile ilizindua simu yake ya kwanza yenye ‘Dual front led flash’ , simu hiyo inaitwa Tecno Camon CX.  Mnamo Agosti 2017, Tecno Mobile ilizindua mfululizo wa ‘SPARK’ kwa kutoa simu mbili Tecno Spark K7 na TECNO Spark K9.

Kampuni hii ina undugu wa karibu na simu za Itel, Infinix na kampuni ya kutoa huduma baada ya mauzo kwa wateja ya CARLCARE International.

SOMA NA HII:  Kukua Kwa Teknolojia na Kazi 7 Zinazoelekea Kutoweka

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako