Sambaza:

Kama kuna simu ya Tecno yenye betri kubwa yenye uwezo wa kukaa na chaji muda mrefu tofauti na simu nyingine tunazo zifahamu, basi Tecno L8 ndio yenyewe.

Tecno L8 ina uwezo mkubwa wa betri miongoni mwa Smartphones za Tecno. Bila shaka, Simu janja hii haiwezi kulinganishwa na simu nyingine za Tecno ambazo ni high-end. Lakini kwa bei yake nafuu na uwezo wa mkubwa, L8 iko katika ligi yake yenyewe.

Kwa watumiaji wanaozingatia bajeti, utafurahi kuwa kwa bei ya chini kati ya Tsh200,ooo-Tsh280,000 unaweza kuwa na simu ambayo ina sifa bora ambazo unaweza kuzifurahia.

Ikiwa unahitaji chaguo nafuu kuliko L8, angalia Tecno W5.

Hebu tufanye tathmini ya L8:

Tecno L8

FAIDA – Uzuri Wake

  • Umbo zuri na Mwonekano bora
  • Inadumu
  • Nafuu

HASARA – Mapungufu yake

  • Haiunga mkono 4G LTE
SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuflash Simu za Tecno Kwa Kutumia SP Flash Tool

UWEZO NA BEI YA SIMU YA TECNO L8 NCHINI TANZANIA

Mfumo wa Uendeshaji: Android 5.1 (Lollipop)
Processor: 1.3 GHz quad-core MediaTek 6753 Chipset
Memori: 1 GB RAM
Rangi: Rangi mbalimbali
Idadi ya SIM: Inatumia Laini Mbili
Bei yake: Tsh200,000 hadi Tsh280,000

Kioo

Kioo: 5.5-inch Touch Display, 720 x 1280 pixels (267 ppi)

Kamera

Kamera ya Nyuma: 8 MP, LED Flash, Face Detection, Touch Focus
Kamera ya Mbele: 2 MP, LED Flash

Uwezo wa Mtandao

2G: Ndio
3G: Ndio
4G LTE: Hapana

Uhifadhi

Uhifadhi wa Ndani: 32 GB
Sehemu ya Memori kadi: Ndio

Intaneti & Uunganisho

GPRS: Ndio
EDGE: Ndio
3G: Ndio
NFC: Hapana
USB Port: Ndio
Wi-Fi Hotspot: Ndio

Messaging

SMS/MMS: Ndio
Instant Messaging: Ndio

Burudani

Music Player: Ndio
FM Radio: Ndio
Loudspeaker: Ndio
Video Player: Ndio
Headphone Jack: Ndio
Fingerprint Reader: Ndio

SOMA NA HII:  HTC U11 Life: Toleo jipya la simu janja kutoka HTC! #Uchambuzi

Uwezo wa Betri

Betri: 5050 mAh Li-ion Battery

MUUNDO, SIFA KAMILI, NA KIOO

Tecno L8

Imetengenezwa na vifaa bora; L8 imetengenezwa kwa chuma na  plastiki inayowavutia watu wengi sana kwa muonekano wake.

Simu ni nene, hasa pembeni ambao kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya ukubwa wa betri (5050 mAh). Lakini pamoja na uzito, simu hii ni rahisi kuibeba.

L8 ina kioo cha ukubwa wa inchi 5.5 na resolution ya pixels 720 * 1280, ina kioo kikubwa zaidi kuliko simu nyingine za bei ya kati kwenye soko. Je, bajeti yako ni ndogo? kama jibu ni ndio basi angalia simu ya W3 au W4.

KAMERA

Kamera haiko nje ya ulimwengu huu. Bila kujali, kamera ya nyuma yenye megapixel 8 ni nzuri na inatosha kupigia picha zenye ubora wakati MP 2 upande wa mbele ni kwajili ya kuchukua selfies na video calls.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu Mpya ya Tecno Camon CM Bei na Sifa Zake

Wakati hatuwezi kuoga nyumba ya kamera kwa sifa, bei ya simu inathibitisha ubora wa kamera.

PROGRAMU

Processor ya Tecno L8 inafanya simu kuwa juu ya simu nyingi unaziona leo. Inatumia quad-core processor yenye kasi ya 1.3 GHz na 1 GB ya RAM, L8 ni nyepesi unapoitumia, na inafanya kazi vizuri.

Ingawa GB 1 inaweza kuwa tatizo kwa watumiaji wengi wa simu wanaopenda kutumia programu nzito/kubwa, msaada wa 1.3 GHz hutoa kasi unayohitaji wakati unatumia simu.

BETRI

Betri yake ni Cream De La Cream. Bila shaka, 5050 mAh ni ubora unaoweza kupata kutoka kwenye simu za Tecno. Kwa betri ya 5050 mAh, L8 ni nzuri kwa watumiaji wanaopenda kutumia simu kwa muda mrefu.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako