Sambaza:

Tecno Camon C8 vs Tecno Boom J8 – Ni simu gani ninunue kati ya hizi ? Katika makala hii, tutazungumza kiundani kuhusu simu janja zote mbili kutoka Tecno kwa kufananisha uwezo, utofauti , ubora na matatizo ya kila simu.

simu gani

Tecno Boom J8 ilizinduliwa Machi 2016 kama kuboreshwa kwa Tecno Boom J7. Ina kioo chenye inchi 5.5, uwezo wa RAM WA 2GB na inatumia mfumo wa uendeshaji wa Android 5.1 Lollipop.

Tecno Camon C8 ilizinduliwa Agosti 2015 na ina skrini ya inchi 5.5 , uwezo wa RAM wa 1GB RAM na kamera yenye 13MP.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Itel S32 na Itel S32 LTE bei na Sifa zake

Tecno Camon C8 vs Tecno Boom J8 – Kufanana Kwao na Utofauti

Kufanana:

 • Zote zinatumia laini mbili
 • Zote zina skrini yenye ukubwa wa inchi 5.5
 • Zote zina kamera ya nyuma ya13MP na kamera ya mbele ya 5MP
 • Zote zina hifadhi ya ndani (Internal Storage) ya 16GB
 • Zote zinatumia toleo la Android 5.1 Lollipop Os
 • Zote zina betri yenye ujazo wa 3000mAh.
 • Zote zina betri ambayo haitoki

Utofauti :

 • Camon C8 ina 1GB RAM wakati Tecno J8 ina 2GB RAM
 • Camon C8 haina uwezo wa 4G LTE wakati Tecno J8 inatumia mtandao wa 4G.
 • Tecno C8 haina uwezo wa kuchaji kwa haraka. Tecno J8 inakuja na uwezo wa kuchaji kwa haraka.
SOMA NA HII:  Jinsi ya kuongeza kasi ya simu yako ya Android

Sifa Muhimu za Tecno Camon C8 :

 • Idadi ya Laini: Inatumia laini mbili
 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 5.1 (lollipop)
 • Kioo: 5.5 inches
 • RAM: 2 GB
 • Hifadhi ya Ndani: 16 GB
 • Kamera ya Mbele: 5.0 MP na LED Flash
 • Kamera ya Nyuma: 8.0 MP na LED Flash
 • Betri: 3000 mAh

[Soma Zaidi Kuhusu Camon C8]

Sifa Muhimu za Tecno Boom J8

 • Mfumo wa Uendeshaji: HiOS (Android 5.1)
 • Uwezo wa Mtandao: 2G, 3G, 4G.
 • Ukubwa wa Kioo: Inchi 5.5 pamoja na kioo chenye teknolojia ya IPS.
 • Uwezo wa Processor: Quad-core
 • Uwezo wa RAM: 2GB
 • Ukubwa wa Ndani: 16 GB.
 • Ukubwa wa Nje: microSD, mpaka ukubwa wa 128GB
 • Kamera ya Nyuma:  13.0 MP AF
 • Kamera ya Mbele: 5.0 MP na Flash
 • Uwezo wa Battery: 3000 mAh huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Li-Ion
SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Gionee F205 Bei na Sifa Zake

[Soma Zaidi Kuhusu Tecno Boom J8]

Sasa turudi upande wako. Ni simu janja gani unafikiri ni bora zaidi? Toa maoni yako !!

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako