Ifahamu simu ya Tecno Boom J8 bei na Sifa zake


Simu ya Tecno Boom J8 ilipokelewa vizuri sana kutokana na ubunifu na upatikaji wake katika bei iliyokuwa ya nafuu ukilinganisha na simu zenye sifa kama yake kutoka makampuni mengine.

Tecno Boom J8

Sifa na Uwezo wa Tecno Boom J8 kwa ufupi

  • Programu endeshaji: Android 5.1 spesheli ya HiOS
  • Teknolojia za mawasiliano: 2G/3G/4GLTE (GSM/WCDMA/LTE) ( LTE:Band B3/7/20)
  • Prosesa: Quad-core
  • Kioo (Display): Inchi 5.5 HD IPS Touchscreen
  • Kamera: Megapixel 13 nyuma, MP 5 mbele (selfi), zote zinapiga Flash
  • Diski ujazo (storage): GB 16GB pamoja na RAM ya GB 2
  • Uwezo wa betri: mAh 3000
  • Teknolojia zingine – Wi-Fi, BT, GPS
  • Unaweza tumia memori kadi (Micro SD) ya hadi GB 128

Android 5.1 – HiOS

Simu hii inakuja na toleo la programu endeshaji la Android 5.1 lakini lilofanyiwa maboresho ya muoneakano uliopewa jina la HiOS. Muonekano huu wa HiOS ukijumlisha na RAM ya GB 2 iliyokwenye simu hii inaifanya simu hii kuwa na kasi nzuri katika utendaji wake.

 Muonekano

Ukiishika kwa mara ya kwanza lazima utakubali ya kwamba simu hii ni maboresho makubwa kutoka Tecno Boom J7. Boom J8 ni nyembamba na inastahili sifa ya kuwa kati ya simu janja nyembamba zaidi za ukubwa wa inchi 5.5.

Kutengeneza kasha lake (housing) imetumika plastiki pamoja na aluminiamu ambayo inasaidia kuipa simu muonekano wa kuvutia.

Kamera

Kwenye Tecno Boom J8 kuna maboresho kadhaa kutoka toleo la J7. J8 inakuja na kamera ya nyuma ya MP 13 na ya selfi MP 5, ukilinganisha na J7 ambayo ilikuwa na kamera ya nyuma ya MP 8 na ya selfi ikiwa ni MP 2.

Kamera zimekuja na teknolojia ya maboresho ya ubora wa picha – optical image stabilization. Pia kamera ya nyuma inauwezo wa kupiga picha za panorama. App ya kamera ina uwezo wa kutambua (‘detect’) sura na pia inakupa nafasi ya kuboresha vitu kama mwanga n.k kabla ya upigaji picha.

Ukaaji wa Chaji (Betri)

Katika majaribio niliyofanya nilifanikiwa kuangalia muvi mbili kupitia app ya VLC niliyoipakua pamoja na kusikiliza muziki kwa zaidi ya masaa mawili na bado nikawa na kiwango cha chaji cha zaidi ya asilimia 40%.

Tecno Boom J7 ilikuja na betri ya mAh 2020 wakati Boom J8 imeongezwa maradufu kiwango cha betri na kufikia mAh 3000. Kwa kipimo hichi utaweza kufanya mambo mengi ndani ya siku bila ya kuwa na wasiwasi na suala la chaji. Pia kupitia uwezo wa ‘Ultra lower power mode’ utaweza kufanya simu yako kutumia kiwango kiduchu zaidi cha chaji kwa apps muhimu tuu pale unapojua utakuwa mbali na uwezo wa kuchaji kwa muda mrefu.

Tecno Boom J8 pia imetengenezwa kwa teknolojia za juu za mfumo wa sauti – hivyo iwe kupitia spika za simu yenyewe au pale unapotumia headphones kiwango kizima cha sauti kinachotoka ni cha kiwango cha juu. Boom Player kama app spesheli ya simu hii ipo katika uwezo mkubwa wa kutumia teknolojia hizi kuhakikisha kiwango cha uchezaji muziki ni cha juu.

Bei:

Wakati Boom J8 imekuja na maboresho mengi bado bei yake haijaenda mbali sana na ile iliyokuja na Boom J7, simu ya Boom J8 inapatikana kwa kati ya Tsh 380,000/= hadi Tsh 450,000/=, hivyo kama ni bajeti basi ukiwa na Tsh 400,000 unaweza ukawa poa. (Kwa Kenya Ksh 14,999/- Ksh 16,999/=)

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA