Sambaza:

Simu ya Tecno Boom J7 vs Boom J8 – Kuna tofauti gani ? Je, natakuwa kununua simu mpya ?. Jiunge nasi katika makala hii. Hapa, tutafananisha simu janja zote mbili kulingana na jinsi zinavyofanana na tofauti zao.

Simu ya Tecno Boom J8 inapatikana kwenye soko, na  Watanzania wengi wamekuwa wamekuwa wakijiuliza kama kuna tofauti yoyote ya msingi kati ya Boom J8 na J7. Naam, kulingana na sifa, Boom J8 ni bora kuliko J7.

boom boom


Tecno Boom J7 vs Boom J8

Hapa, tutafananisha simu janja zote mbili kwa kulingana vitu vinavyofanana na tofauti zao.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuflash Simu za Tecno Kwa Kutumia SP Flash Tool

Kufanana Kwao :

 • Zote zinatumia laini mbili (Dual SIM)
 • Zote zina  720 x 1280 pixels screen resolution.
 • Zote zina hifadhi ya ndani (internal memory) 16GB
 • Zote zina chipset maalum kwajili ya muziki

Tofauti Zao :

 • Boom J7 ina 1GB RAM – Boom J8 ina2GB RAM
 • Boom J7 ina skrini inchi 5  – Boom J8 ina skrini inchi 5.5
 • Boom J7 ina kamera ya nyuma ya 8MP – Boom J8 ina kamera ya nyuma ya 13MP
 • Boom J7 ina kamera ya mbele yenye 2MP  – Boom J8 ina kamera ya nyuma ya 5MP
 • Boom J7 inatumia Android KitKat – Boom J8 inatumia Android 5.1 Lollipop na TECNO HiOs interface
 • Boom J7 ina betri yenye ujazo wa 2020mAh – Boom J8 ina betri yenye ujazo wa 3000mAh
 • Boom J7 haina uwezo wa kuchaji haraka – Boom J8 ina uwezo wa kuchaji haraka
 • Boom J7 inakuja na earpiece – Boom J8 inakuja na headset
 • Boom J7 haina uwezo wa 4G – Boom J8 inatumia mtandao wa 4G.
SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Infinix Note 4 Pro na sifa zake

Kama unavyoona , Tecno Boom J8 ni maboresho makubwa ya J7. Ina RAM zaidi , ujazo mkubwa zaidi wa betri  (na uwezo wa kuchaji haraka) na kitu cha muhimu zaidi , ina uwezo wa 4G LTE.Kwa hiyo kama unatumia J7 na unataka kuhamia kwenye J8 ,ni jambo zuri.

Sasa turudi upande wako , unaionaje simu ya Tecno J8? Tuambie mtazamo wako. Unaweza kusoma uchambuzi kamili wa simu ya J8 : Ifahamu simu ya Tecno Boom J8 bei na Sifa zake.

Want to buy the Boom J8? Use the link below-

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako