TCRA: Nyimbo Hizi 13 za Bongofleva Zisipigwe Kwenye Radio na TV


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza rasmi leo February 28, 2018 marufuku kwa vyombo vya habari nchini kupiga nyimbo 13 za bongofleva ambapo mamlaka hiyo imedai kuwa nyimbo hizo hazina maadili.

Barua kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania imeeleza kuwa ilipokea orodha ya nyimbo hizo kutoka kwa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ambalo limeeleza kua nyimbo hizo ni kinyume na maadili na kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) 2005.

Baadhi ya nyimbo hizo zilizofungiwa ni pamoja na Wakawaka na Hallelujah za Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Kibamia wa Roma Mkatoliki, Hainaga ushemeji wa Amani Hamis maarufu kama Manfongo, Nyimbo mbili za Ney wa Mitego, jina lake halisi Emmanuel Elibariki – Pale kati Patamu na Maku Makuz – pia zimefungiwa.

Nyimbo zingine ni I am Sorry JK wake Nikki Mbishi ambaye jina lake halisi ni Nicas John Mchuche, Chura na Nimevurugwa za Snura Mushi maarufu kama Snura na nyingine.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA