TCRA imezindua mfumo wa usajili laini kwa kutumia alama za vidole


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua mfumo wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole (Biometric). Mfumo huo umezinduliwa leo March 1, 2018 na utatumika kuhakiki taarifa za wateja wapya wa kampuni zote za simu Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi  huo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Engineer James Kilaba ametaja mikoa sita nchini kuanza utekelezaji wa zoezi la kusajili laini za simu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole.

Mikoa hiyo kuwa ni Dar es salaam, Pwani, Iringa, Tanga, Singida na Zanzibar pia amesema huduma hiyo inatokana na changamoto wanazokutana nazo katika swala zima la usimamiaji wa huduma hiyo.

Ameeleza kuwa kutokana na tabia iliyozuka juu ya udanganyifu hasa katika kutoa taarifa za wanaosajili namba zao huku baadhi wakitumia simu kufanya uhalifu.

”Kutokana na changamoto hizo za kuongezeka kwa watumiaji wa huduma hii kuna umuhimu wa kuwa na takwimu sahihi za watumiaji kwa ajili ya matumizi ya usiamamizi, kiuchumi na kiusalama” amesema Engineer James Kilaba.

Aidha ameongezea kuwa mfumo huo pia utawezesha kuhusu watumiaji wa simu za mkononi kwa ajili ya kuweka mipango ya kuendeleza sekta ya mawasiliano.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA