TCRA Kutoa Hatima ya Diamond Platinumz, Times Fm Wiki Hii


Kamati ya maudhui ya TCRA iliyokuwa ikifanya uchunguzi wa mahojiano waliyoyafanya kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam na mwanamuziki Diamond Platinumz inakaribia kumaliza kazi hiyo na hatima yake itajulikana wiki hii.

Diamond Platinumz

Machi 22, 2018, Times ilipokea barua ya kuwataka wawasilishe kipindi hicho kilichorushwa Machi 19, 2018 kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mwanamuzi Diamond alimlalamikia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kwa kutowatendea haki wasanii baada ya nyimbo za wasanii mbalimbali kufungiwa.

Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Andrew Kisaka ameieleza MCL Digital leo kwamba tayari kamati ya maudhui inakaribia kumaliza kazi yake ya kupitia maudhui ya kipindi hicho.

Amesema mwanamuziki Diamond pia amehojiwa na kwamba majibu ya kilichobainika yatatolewa ndani ya wiki hii.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA