Sambaza:

Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), imefanya uzinduzi wa tovuti ambayo itawawezesha wafanya biashara nchini kufanya biashara kwa njia ya mtandao jambo litakalochangia ukuaji wa biashara zao.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa TCCIA, Makamu wa Rais wa TCCIA, Joseph Kahungwa amesema kupitia tovuti hiyo wafanya biashara ambao ni wanachama wa TCCIA na wasio wanachama watapata nafasi ya kuweka biashara zao katika tovuti hiyo na zitaweza kuonekana duniani kote na hivyo kutawapa nafasi ya bidhaa zao kuonekana sehemu yoyote.

Amesema katika soko la sasa la utandawazi tovuti hiyo itawasaidia wanachama kutangaza bidhaa zao na watakuwa katika hatua nzuri ya bidhaa kuonekana na wafanya biashara kutoka nchi zingine na hata kupata wateja kutoka nchi zingine na hivyo kujiongezea kipato.

“Biashara ya dunia ya sasa imekua na kufanyika kwenye mtandao na hivyo tovuti hii itaweza kusaidia kupata wateja wapya kutoka mataifa mbalimbali na hata kukutana na wafanya biashara kutoka mataifa mengine,” alisema Kahungwa.

Makamu wa Rais wa TCCIA, Joseph Kahungwa akizungumza kuhusu tovuti hiyo ambayo itawawezesha wafanya biashara kuweka bidhaa zao mtandaoni wakati wa warsha ya uzinduzi wa mtandao huo.

Nae mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), Stella Karegyesa amesema UNV iliamua kushirikiana na TCCIA sababu ya kutambua umuhimu wa kufanyika kwa biashara kwa njia ya mtandao.

SOMA NA HII:  Wanafunzi wa Primary Tanga kuanza kusoma kwa kutumia Tablet

Alisema UNV wanaamini kupitia tovuti hilo wafanya biashara watakuwa katika nafasi nzuri ya kutanua biashara zao kwa sababu ya kuwa katika sehemu ambayo itawawezesha kukutana na watu wapya katika biashara ambao watashirikiana nao kufanya kazi.

“Tovuti hii imeanzishwa ili kusaidia wafanyabiashara wa Tanzania na sasa wataweza kuonyesha bidhaa walizonazo kimataifa ni hatua nzuri kukuza biashara wanazofanya,” alisema Bi. Karegyesa.

Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akisoma hotuba ya UNV kuhusu tovuti hiyo.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Consolatha Ishebabi aliyemwakilisha waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji amesema ni fulsa nzuri kwa wafanyabiashara wa Tanzania lakini wafanye marekebisho katika lugha zilizopo katika tovuti hiyo waweke na Kiswahili ili hata wafanyabiashara waioelewa Kiingereza waweze kutumia Kiswahili ambacho ndiyo lugha mama nchini.

Mwakilishi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Consolatha Ishebabi akielezea jinsi serikali itakavyoshirikiana na TCCIA ili kusaidia wafanya biashara kupata masoko zaidi kimataifa na faida za tovuti hiyo.

Nae Mtaalam wa IT wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), Puspa Raj amesema kupitia tovuti hiyo wafanyabiashara wa Tanzania bidhaa zao zitaonekana kwa watumiaji wa intaneti zaidi ya Bilioni 3 duniani kote na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuongeza kipato cha biashara wanazofanya.

SOMA NA HII:  Baada ya Kauli ya JPM, Ifahamu Sheria ya Takwimu na Madhara Yake

Mtaalam wa IT wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), Puspa Raj akielezea jinsi tovuti hiyo itakavyofanya kazi na fulsa watakazopata wafanya biashara.

TCCIA imezindua tovuti hiyo itakayowawezesha wafanya biashara kuweka bidhaa katika mtandao huo kwa msaada wa UNV, UNDP na Serikali ya Japan ambapo wafanya biashara watakuwa wakiweka bidhaa bure katika tovuti hiyo ya tccia.com/edirectory

Mwenyekiti wa TCCIA wilaya ya Temeke, Paulo Koyi akitoa neno la ukaribisho katika warsha hiyo ya ufunguzi wa tovuti.

Baadhi ya wanachama wa TCCIA waliohudhuria katika uzinduzi wa tovuti ya tccia.com/edirectory

Mwakilishi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Consolatha Ishebabi (aliyeketi) akifanya uzinduzi wa tovuti, (wa kwanza kulia katika waliosimama) Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, Magdalene Mkocha, Mtaalam wa IT wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), Puspa Raj, Makamu wa Rais TCCIA anayeshughulikia viwanda, Yakub Hasham na Makamu wa Rais wa TCCIA, Joseph Kahungwa.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako