Magari

Taxify: Huduma mpya ya usafiri iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam

on

Taxify ni  App ya huduma ya usafiri inayokuwa kwa kasi barani Ulaya na Afrika, imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam huku mamia ya madereva wakijiorodhesha ili kuanza kutoa huduma hiyo katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Taxify

Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify Kanda ya Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa App hiyo leo jijini Dar es salaam.  Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka.

Katika kusherehekea uzinduzi wa huduma hiyo mpya, ambayo inakua kwa kasi barani Ulaya na Afrika Taxify imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma hiyo kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi.

SOMA NA HII:  Magari 5 Maarufu Kwenye Movie na Uwepo Wake kwa Sasa

Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa Sh 600, Sh300 kwa kila kilometa moja, Sh 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Sh 3000.

Mwigizaji wa Bongomovie Wema Sepetu amechaguliwa kuwa Balozi wa huduma hii.

“Dar es Salaam ni jiji lenye soko kubwa na lenye faida kwa usafiri wa watu binafsi mijini na sehemu muhimu ya shughuli za kibiashara ambapo shida kubwa ya kutumia usafiri binafsi maeneo ya mjini hutokea.

Tunayofuraha kubwa kuzindua huduma hii hapa na tuna uhakika Taxify itasaidia kwa kiasi kikubwa kuchangia kwa ufanisi katika ushindani wenye afya na kuboresha ubora wa huduma huku tukitoa kutoa fursa kwa madereva kujipatia kipato kizuri,” alisema Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Kanda, Taxify.

SOMA NA HII:  Kufikia 2040 China itakuwa imefikia hatua hii ya teknolojia ya magari

Taxify inachukua asilimia 15 pekee ya mapato kutoka kwa madereva wake, ikiwa ni gharama ndogo zaidi ukilinganisha na washindani wetu wa kibiashara wanaochokua asilimia 25.

Taxify tayari inatoa huduma zake kwenye nchi 20 duniani na imeonyesha mafanikio makubwa kutokana na huduma zake nafuu na uwazi katika uendeshaji.

Taxify inapatikana kwenye mfumo wa IOS na Android.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.