Tanesco Yafafanua Kuhusu Kununua Umeme Kwenye Simu


Mtandao wa Vodacom hivi karibuni ulitangaza kusitisha huduma ya kununua umeme wa LUKU kupitia MPESA, lakini kujitoa huko hakukudumu kwani baadae kampuni ya Vodacom Tanzania ilitoa tamko na kusema itaendelea na huduma hiyo na badala yake kutakuwa na ongezeko la malipo ya kupewa huduma hiyo ya LUKU ambayo yatakuwa asilimia 1.1.

Baada ya kuwepo kwa sintofahamu kwa wateja kuhusu ongezeko la asilimia hizo 1.1, hivi leo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limezungumzia na kutoa ufafanuzi kuhusu tozo ya asilimia 1.1 wanayokatwa wateja baada ya kununua umeme kwa njia ya mitandao ya simu na pia kwa kupitia kwa mawakala wa benki.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA