Home Nyingine Tamko la BASATA kuhusu wimbo wa Nikki Mbishi ‘I’m Sorry JK’

Tamko la BASATA kuhusu wimbo wa Nikki Mbishi ‘I’m Sorry JK’

0
0

Baada ya wimbo wa ‘I’m sorry JK‘ uliofanywa na Nikki Mbishi kufungiwa na baraza la sanaa Tanzania (BASATA). Nikki kupitia mtandao wa Instagram aliandika

“Kwa yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa, hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria“

“Naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia” – Nikki Mbishi

Baada ya maneno hayo Baraza la sanaa Tanzania leo (BASATA) limetoa tamko kupitia ukurasa wao wa Twitter :

“Nikki Mbishi aliitwa kwa mashauriano ya kazi za sanaa ambapo alibaini kwamba wimbo wa ‘I’m Sorry JK’ una kasoro, kaona ausitishe“

“Tunampongeza kwa kubaini mapungufu na kuchukua hatua stahiki, tunatoa wito wa kubuni maudhui yenye staha na yasiyo chonganishi” – BASATA

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *