Baada ya kamati ya utendaji wa Yanga kupitia mjumbe wa kamati hiyo Salum Mkemi kutangaza kupinga rufaa ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kwa kumtumia mchezaji Mohamed Fakih aliyedai kucheza dhidi ya Simba akiwa kaoneshwa kadi tatu za njano, Simba kupitia afisa habari wao Haji Manara wametoa taarifa kwa vyombo vya habari.

11-4-2017. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Leo mchana huu kunatembea taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga inayoonyesha kuishinikiza Bodi ya ligi kutokutenda haki juu ya rufani yetu dhidi ya klabu ya Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohammed Fakih aliyecheza dhidi yetu akiwa na kadi tatu za njano ambalo ni kosa kisheria.

SOMA NA HII:  Hali ni mbaya sana kwa tovuti za Pirates na wazee wa Torrent

Taarifa hiyo ya Yanga iliyomnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Salum Mkemi aliyeongea mbele ya waandishi huku akiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa iliitaka bodi kutokutoa points kwa Simba eti kwa kuwa hizo points zitawaathiri Yanga kwenye kutetea ubingwa wao ambao kwa sasa upo rehani.

Taarifa hiyo imeonyesha Yanga wanao ushahidi kuwa Fakih ana kadi mbili za njano. Klabu ya Simba inawaambia viongozi wa Yanga wanayo mambo ya msingi ya kuwashughulisha, ikiwepo kutafuta mishahara ya wachezaji wao iliokwama kwa miezi kadhaa kama inavyoripotiwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuepuka Makosa 5 Yanayofanywa na Wamiliki wa Website

Waangalie namna bora ya kuurejeshea hadhi uwanja wake wa mazoezi wa Kaunda ili upate kuchezeka tena na sio ulivyo hivi sasa,ambapo umegeuka kama bwawa la kufugia kambale ni kushangazwa kulikochupa mpaka kufuatilia rufani isiyowahusu hii ni rufani ya Simba dhidi ya Kagera sio wao Yanga.

Tunaamini bodi haitafanya maamuzi kwa shinikizo la yoyote yule,na hatutarajii kuona porojo walizozisema leo zitaondoa ukweli uliopo mezani kwao ambao klabu yetu imeuwasilisha Mwisho niwaombe washabiki wetu watulie na waiachie bodi ifanye maamuzi yake ambayo tunaamini yatatoa haki kwa anayestahili.
IMETOLEWA NA.. Haji S Manara
Mkuu wa Habari wa Simba Sc
SIMBA NGUVU MOJA @simbasctanzania@mkemi1_supermarket

SOMA NA HII:  Teknolojia 5 Maarufu kwenye Magari Kwa Sasa

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako