Nyingine

Taarifa ya Serikali kuhusu kushambuliwa kwa waandishi kwenye vurugu za CUF

Watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Prof. Ibrahim Lipumba walivamia mkutano wa wafuasi wa Maalim Seif Sharif Hamad na kuwajeruhi wenzao pamoja na waandishi wa habari, Juzi April 22 2017.

Leo Serikali imetoa taarifa kuhusu tukio hilo ambapo Mkurugenzi, Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema:

“Tumechukua muda kidogo kulifuatilia suala hili na kubaini licha ya baadhi ya waandishi kujeruhiwa na kuripoti polisi, wapo ambao vifaa vyao vya kazi vililengwa katika shambulizi hilo.

“Ifahamike kuwa uandishi wa habari ni taaluma adhimu na nadhifu inayopaswa kuheshimiwa, kuenziwa, kulindwa na kutoingizwa katika migogoro ya pande zinazofarakana katika jamii.” – Dkt. Hassan Abbas.

SOMA NA HII:  Kuwa mkweli! Jina gani umetumia ku-save namba ya simu ya mama yako?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.