Sambaza:

Serikali imemwondoa nchini Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo.

Mkurugenzi huyo raia wa Gambia, aliyeletwa nchini na Umoja wa Mataifa (UN) Agosti 2015, aliondolewa wiki iliyopita ndani ya saa 24 kwa agizo la Serikali, huku akiwa chini ya ulinzi.

Akizungumzia kuondolewa kwa kiongozi huyo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Aziz Mlima, alisema kuwa kulitokana na kuibuka kwa mgogoro kati yake na wafanyakazi wa UNDP waliopo nchini.

Dk. Mlima alisema baada ya kuibuka kwa mgogoro huo, Serikali iliamua kuandika barua Umoja wa Mataifa ikitaka kuondolewa kwa mkurugenzi huyo.

“Unajua unapokuwa na kiongozi kama huyo ana kinga ya ubalozi, ni lazima ufuate taratibu na si vinginevyo, hivyo baada ya tukio hilo tuliandika barua kati ya Aprili 6 au 7 na kuomba kuondolewa kwa kiongozi huyo.

“Na kikubwa unapokuja katika nchi kama yetu ni lazima ushirikiane na Serikali iliyopo na si vinginevyo na kwenda kinyume ni sawa na ukwamishaji wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2020. Na UNDP ni mbin mkubwa wa maendeleo kwa nchi yetu, ila kama unakuja tofauti na maelengo na kazi za UNDP, huku ni kuleta mgogoro,” alisema Dk. Malima.

Alisema mara nyingi Serikali imekuwa ikitoa heshima zote kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwamo UNDP, lakini pindi inapobainika yanakwenda kinyume na malengo ya kazi, katu Serikali haiwezi kuruhusu hali hiyo.

Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi kuhusu Serikali kumuondoa nchini, Mkurugenzi wa UNDP, Bi. Awa Dabo.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako