Nyingine

Swali!! Unafikiri nani anapaswa kulaumiwa kwa mimba za utotoni ?

Kumekuwa na ongezeko kubwa la mimba za utotoni na kuna masuala mengi yanahusishwa na jambo hili.

Mimba na ndoa za utotoni ni miongoni mwa vikwazo vinavyowapata watoto wa kike wa Tanzania, tatizo ambalo bado ni kubwa katika baadhi ya maeneo ya Tanzania Bara na Visiwani.

Baadhi ya watu hupeleka lawama kwa wazazi wa wasichana, jamii, Mitandao ya kijamii , kundi rika, wasichana wenyewe na wanaume ambao huwapa hawa watoto ujauzito.

Unafikiri nani anapaswa kulaumiwa kwa mimba za utotoni zinazotokea katika jamii zetu?

Ni nani wa kuwafichua watuhumiwa na kukomesha ouvu huo, nani wa kumfunga paka kengele?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *