Sambaza:

Mnamo Septemba 14, 2017, BANK OF AFRICA- TANZANIA ilianzisha app yake mpya ya benki inayoitwa “SWAHIBA Mobile” kwenye soko la Tanzania katika Jiji la Dar es Salaam.

Hii imefuatia kupitishwa/kuboreshwa kwa huduma zake za “B-Mobile banking services”, ambayo inaruhusu watumiaji kufurahia huduma kamili za benki kwa kutumia simu ya mkononi.

Inakuja na sifa nyingi mpya na kazi; App ya SWAHIBA inawapa wateja jukwaa moja kwa ajili ya ushirikiano wote na huduma zinazotolewa na benki. Wateja wanaweza kufikia akaunti zao za kibinafsi na biashara kila mahali, kwa wakati mmoja.

Kazi ya App inajumuisha uhamisho wa fedha, huduma za hundi, maombi ya mkopo wa papo hapo, malipo ya bill, kutoa pesa bila kadi ya ATM , kununua salio la simu, usajili wa Huduma za benki kwa njia ya Simu za mkononi na huduma za e-chama na huduma nyingine nyingi.

Zaidi ya hayo, mtu yeyote ikiwa ni pamoja na wateja wasiokuwa wa BANK OF AFRIKA wanaweza kufanya huduma bila ya kujiunga na huduma kama vile Bidhaa za BOA na ofa, Maombi ya Mikopo, Kujua tawi la BOA na ATM, ununuzi wa mtandaoni na ubadilishaji viwango vya fedha za kigeni.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa bank of Africa Ammishaddai Owusu-Amoah alisema kuwa Benki hiyo inajivunia kuanzisha programu yake mpya ya benki ya mkononi (mobile banking App) wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya benki.

SOMA NA HII:  Mbinu ya kuongeza uaminifu kwa wateja kwa kutumia Email za kibiashara

“Uzinduzi wa SWAHIBA Mobile App huonyesha shukrani zetu kubwa kwa wateja wetu wote wenye thamani kwa imani yao katika benki yetu, kwa jamii, washirika na wadau wote, katika kipindi cha miaka 10 ya kazi nchini. “Inasisitiza ahadi yetu ya kuweka mapendeleo ya wateja wetu kwanza na kubadilisha kutoa huduma za kisasa kwa wateja. Pia inathibitisha uamuzi wa benki wa kujenga uwepo wake wa benki ya digital na kukidhi mahitaji ya haraka ya wateja wetu ” alisema Ammish.


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako