Nyingine

Sumaye: Rais anatakiwa kutii hisia za wananchi wake.

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema Rais John Magufuli amesahau kama amechaguliwa na wananchi jambo linalomfanya kufanya maamuzi yake bila kujali hisia zao.

Sumaye alitoa kauli hiyo Jumanne hii jijini Dar es Salaam alipozungumza na wanahabari katika ofisi za Kanda ya Pwani za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , kufuatia kauli za Rais Magufuli alizotoa kuwa haelekezwi kufanya mambo yake kwani alichukua fomu peke yake, hivyo hakuna anakayemuelekeza katika maamuzi yake.
Sumaye ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chadema, amesema, anakubaliana na Rais kuwa ana mamlaka ya kupanga watu wake na hakuna mtu anayeweza kumuingilia katika hilo lakini anatakiwa kutii hisia za wananchi wake.

“Nimemsikia Rais akisema kwamba yeye haambiwi, yeye ndio Rais, ni kweli, akasema alichukua fomu ya kugombea urais yeye peke yake kwa hiyo anatenda kazi zake anavyotaka, ni kweli lakini ni nani alimpigia kura? Ni watanzania ndiyo waliomfikisha pale,” amesema Sumaye.

Amesema, haki itendeke kwenye jambo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusishwa na tuhuma mbalimbali na kuwa limezungumziwa na rais, mawaziri na inaonekana mikanganyo ya dhahili na inaonekana pia kuna mtu anabebwa.

“Kama mkuu wa mkoa anafikia mahali anavamia kituo cha habari, waziri anayehusika na habari anakwenda anasikitika, lazima kuna tatizo, mimi Makonda nikisikia hata kesho ameingia mahali amepiga watu makofi wala sitashangaa, ametukana watumishi mbele ya kadamnasi sishangai, kwa sababu kama kweli yale yaliyoandikwa ni kweli, amefika mwisho wa uwezo wake,” amesema.

 

SOMA NA HII:  Marufuku Matumizi ya Takwimu za Kampuni ya Geopoll - Dkt. Mwakyembe

Zinazohusiana

JIUNGE NA MAZUNGUMZO, TOA MAONI YAKO HAPA

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Lako