Sambaza:

Waziri Kivuli wa Habari Utamaduni na michezo Mhe Joseph Mbilinyi anaongea na waandishi wa habari muda huu kuhusu kupotea kwa Msanii Roma. Baada ya kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paulo Makonda kusema msanii pamoja na mwenzake wanaweza kupatikana kabla siku ya jumapili

“Wananchi wanahoji Roma na wenzake wako wapi sababu hawajui, lakini mtu anayejua walipo amesema watapatikana Jumapili.”

“Jana alisema hadi Jumapili Roma na wenzake watakuwa wamepatikana, sisi tunamtaka awaachi leo warudi kwenye familia zao.”
“Akisema atawatoa Jumapili, ni kazi gani amewapa ambayo anajua hadi siku hiyo watakuwa wamemaliza, atueleze.”

“Badala ya Wizara ya Habari kuomba ushirikiano wa wananchi, wamchukue huyo anayejua walipo. Mtu asiogope kupoteza uwaziri”

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako