Magari

Stori ya mlango wa ndege iliyokuwa angani kuangukia nyumba

on

Familia moja nchini India imepigwa na mshangao baada ya mlango wa ndege kuangukia nyumba yao katika mji ulio kusini mwa India wa Hyderabad.

Mwanamume ambaye alikuwa akipaka paa la nyumba rangi aliponea baada ya kwenda kupata chakula cha mchana wakati kisa hicho kilipotokea,

Ndege hiyo ya kubeba abiria wanne ambayo ni ya kutoa mafunzo ilikuwa ikiruka chini chini.

Aliongoza kuwa rubani na mwanafunzi wake wako salama na uchunguzi umeanza kubaini ni vipi kisa hicho kilitokea.

Insepkta wa Polisi Karan Kumar Singh alisema kuwa ni kawaida kuona ndege zikiruka chini chini eneo hilo.

SOMA NA HII:  Amazing! Angalia Muonekano wa Barabara Mpya Iliyojengwa China (Picha)

Rubani na mwanafuzi wake waliponea mwezi Septemba wakati ndege kama hiyo ilipoanguka katika eneo hio.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.