Nyingine

Stori tano kubwa kwenye michezo May 5, 2017, Ni kuhusu UEFA, Mourinho, Barcelona, FIFA na Chelsea

UEFA yapanga kubadili utaratibu wa penalti

Chelsea walishindwa na Manchester United fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2008 wakipiga penalti wakiwa wa pili

Shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA Lipo katika mikakati ya kufanya majaribio mfumo mpya wa upigaji wa mikwaju ya Penalti mitano mitano ili kuondoa faida ya timu inayoanza kupiga Penalti hizo.

Badala ya klabu kubadilishana mmoja baada ya mwingine, UEFA inatafakari uwezekano wa kufuata utaratibu sawa na unaofuatwa katika mchezo wa tenisi.

Utaratibu huo unafanyiwa majaribio katika michuano ya ubingwa wa Ulaya kwa wachezaji wa chini ya miaka 17 ambayo ilianza Croatia Jumatano.


Mourinho atangaza kuwapumzisha wachezaji dhidi ya Arsenal

Jose Mourinho amesema kuwa atawapumzisha wachezaji walioshiriki mechi nyingi dhidi ya Arsenal

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa atawapumzisha wachezaji wake katika mechi ya siku ya Jumapili dhidi ya Arsenal.

Ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya klabu ya Uhispania Celta Vigo siku ya Alhamisi ulikuwa wa 10 tangu mwezi Aprili.

Huku kikosi hicho cha Mourinho kikiwa katika nafasi ya tano katika jedwali la ligi ya Uingereza, ligi ya kombe la Europa inaweza kuwapatia fursa ya kushiriki katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao.

Ronald Koeman atamani kuifunza Barcelona

Meneja wa klabu ya Everton, Ronald Koeman, amesema ndoto zake kubwa ni siku moja kuja kuifundisha klabu yake ya zamani ya Barcelona, lakini amesisitiza kwa sasa anahitaji kuhakikisha klabu yake Everton inashiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya kwanza.

Koeman alitumikia nafasi ya Beki katika kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi katika zama zake, na pia aliwahi kukichezea kikosi hicho cha Nou Camp kwa takribani miaka 6, akianzia miaka ya 1989 hadi miaka 1995.

Brazil vinara wa soka Ulimwenguni

FIFA

Shirikisho la kandanda Ulimwenguni Fifa limetoa orodha mpya ya ubora wa viwango vya soka ulimwenguni.

Brazil bado ni vinara kwa nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Argentina nafasi ya pili,nafasi ya tatu ni Ujerumani,nafasi ya Nne ni Chile, nafasi ya tano ni Colombia ,nafasi ya sita ni Ufaransa,nafasi ya saba ni Ubeligiji, nafasi ya nane ni Ureno ,nafasi ya tisa ni Switzerland na nafasi ya kumi ni Hispania.

Kwa upande wa Afrika Misri bado ni vinara ikiwa katika nafasi ya 19 Ulimwenguni, na orodha nyingine ya ubora Duniani itatoka tena Juni Mosi.

Conte awaonya wachezaji wake kutobweteka

Kinyang’anyiro cha ubingwa wa Ligi ya Premier ya England kimepamba moto, ambapo vinara Chelsea wanaongoza na pengo la pointi nne tu dhidi ya nambari mbili Tottenham Hotspurs.

Kocha  wa  viongozi  wa  ligi hiyo Antonio Conte  amewaonya  wachezaji  wake kutobweteka  na  ushindi  wa  mabao 3-0  dhidi  ya  Everton na  kufikiri  kwamba  ubingwa  ni  wao  tu.

Kikosi  cha Conte  kimejiimarisha   katika  nafasi  yake  juu  kileleni mwa  msimamo  wa  ligi, Jumapili, lakini timu  iliyoko katika  nafasi  ya  pili  Tottenham inawafuatia  nyuma  kwa kasi  ya  ajabu

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close