Habari za TeknolojiaNyingine

[Siasa]: Stori tano kubwa kutoka barani Afrika leo May 5, 2017

Zimbabwe ni ya ‘pili’ katika mataifa yaliyoendelea Afrika-Mugabe

Rais Mugabe anasema kuwa Zimbabwe ni taifa la pili kwa maendeleo barani Afrika

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kuwa Zimbabwe ni taifa lililoendelea zaidi barani Afrika baada ya Afrika kusini. Amekana madai kwamba taifa hilo ni tete .

”Tuna takriban vyuo vikuu 14 na asilimia 90 ya watu wamekwenda shule ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi barani Afrika huku akiongezea kwamba uchumi unaimarika.

Jaji aliyetoa matamshi ya kibaguzi ajiuzulu Afrika Kusini

Mabel Jansen alifanyiwa pia uchunguzi na jopo la majaji

 

Jaji mweupe nchini Afrika Kusini amejiuzulu baada ya kutoa matamshi mwaka jana katika mitandao ya kijamii kuwa matukio ya ubakaji ni utamaduni wa watu weusi.

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zenye asilimia kubwa ya matukio ya ubakaji duniani.

Mwanamke ajitokeza kuwania urais nchini Rwanda

Diana Rwagira ni binti wa mfanyabiashara maarufu wa Kinyarwanda Assinapol Rwigara aliyefariki miaka 2

Nchini Rwanda wagombea wa kiti cha urais katika uchaguzi utakaofanyika mwezi wa 8 wanazidi kujitokeza. Diane Rwigara ametangaza rasmi nia yake ya kugombea urais.

Huyu ni Binti wa mfanyabiashara maarufu wa Kinyarwanda Assinapol Rwigara aliyefariki miaka 2 iliyopita katika mazingira ambayo familia yake ilisema ni tatanishi.

Uhuru wa wanahabari bado changamoto Afrika

Huku dunia ikiadhimisha siku ya uhuru wa habari , waandishi habari nchini Uganda wanazidi kukabiliwa na mazingira magumu ya kazi kutokana na sheria kandamizi zinazobuniwa kila kukicha. Aidha makabiliano na vyombo vya usalama hasa polisi na vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa wanasiasa na hata waajiri wao vimeshudiwa mara kwa mara. Haya ni licha ya madai ya utawala nchini humo kwamba unalinda kwa dhati uhuru wa habari.

China yasisitiza ahadi ya kulinda wanyamapori Afrika

Ofisa wa China amesema China itaendelea kutoa uungaji mkono kwa ulinzi wa wanyamapori barani Afrika.

Akizungumza kando ya mkutano wa baraza la Asia na Afrika la sheria za kimataifa AALCO, ofisa wa idara ya usimamizi wa manunuzi na uuzaji wa wanyama na mimea iliyo hatarini Bw. Meng Xianlin amesema, China inaahidi kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na uhalifu dhidi ya wanyamapori.

Serikali ya China na Kenya zimeandaa mkutano maalum kuhusu mapambano dhidi ya biashara haramu ya wanyama na mimea pori, ukiwa kando ya mkutano wa Baraza la AALCO.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *