Stori 10 Maarufu Kuhusu Simu za Mkononi Ambazo Sio za Kweli


Kama kila kitu katika teknolojia, kuna stori nyingi sana za uongo na uvumi kuhusu simu za mkononi na zimekuwepo kwa miaka mingi. Hapa nitazungumzia stori 10 za simu za mkononi ambazo watu wengi wanaamini ni za kweli.

simu za mkononi

Apps ambazo hufanya kazi nyuma ya mfumo zinapaswa kufungwa ili kuokoa betri na kuepuka simu kufanya kazi taratibu.

Apple na Android zote zinawezesha programu kufanya kazi nyuma ya mfumo ili kuboresha mfumo na kuleta ufanisi zaidi. Stori hii inaonekana kama ya kweli kwa sababu ya wazo la kwamba mchakato huu wa ziada hutumia rasilimali za mfumo, na mfumo unapoendesha programu nyingi zaidi, ndivyo simu inavyozidi kuwa nzito kwenye ufanyaji kazi.

Hata hivyo, mifumo yote ya uendeshaji imeweka kiwango cha jinsi programu hizi zinavyoweza kufanya kazi nyuma ya mfumo; Android, chini zaidi kuliko Apple. Lakini kiwango cha nguvu ya betri kinachotumika ni kidogo sana, na kwa kuwa kasi ya simu yako ni muhimu, mifumo yote imeundwa kuwa na uwezo wa kuendesha programu nyingi kwa wakati mmoja.

Athari ya stori hii maarufu ni kuanzishwa kwa task killer apps ambazo zinapatikana kwenye masoko yote mawili. Programu hizi hazina maana, ingawa zinafanya kazi zao za kufunga programu zinazofanya kazi nyuma ya mfumo (background apps), haziokoi kiasi kikubwa kwa upande wa rasilimali, au maisha ya betri. Unachotakiwa kufahamu ni kuwa, Android na iOS watafunga kazi fulani moja kwa moja memori zaidi inapohitajika.

Unapaswa Kuruhusu Betri Yako Iishe kabisa Kabisa Kabla ya Kuchaji Tena

Betri ya Lithium-ion hufanya kazi vizuri zinapoendelea kuwa na chaji. Betri za zamani za NiCAD na NiMH zinakaa muda mrefu unapoacha chaji iishe kabisa kabla ya kuichaji tena kwa asilimia 100. Betri za kisasa hazina tatizo kama hili kwa sababu hazina “cell memory” kama betri za zamani za NiCAD na NiMH.

Hata hivyo, bado kuna ukweli juu ya uvumi huu. Ingawa haifanyi betri yako ikae muda mrefu zaidi, wataalam wengine wanakubaliana kwamba unapaswa kufanya mzunguko wa 0-100 – yaani, acha betri iishe kabisa kabla ya kuichaji tena kikamilifu – kila baada ya miezi mitatu, au baada ya mizunguko 40 ya kuchaji kawaida. Haiongezi maisha ya betri yako, lakini badala yake inaitwa “calibration”.

Bluetooth/Wi-Fi Direct Zinaua Betri Yako

Bluetooth na Wi-Fi Direct hutuwezesha kuhamisha faili kubwa au data nyingine kutoka kwenye kifaa kimoja hadi kifaa kingine kwa njia ya haraka. Wakati tunaweza kujadiliana ipi ni bora zaidi, ukweli ni kwamba zote mbili ni muhimu sana na zinafanana sana. Lakini, Ni kweli zinaua betri lako?

Hapana.

Bluetooth, na Wi-Fi Direct za kizazi cha sasa zinatumia nguvu kidogo sana zinapokuwa hazitumiki. Na mara tu baada ya kuwezesha kifaa kingine na kuanza kuhamisha faili, ndipo zitaanza kula betri yako. Kwa hiyo, kuziwasha tu haiwezi kumaliza betri yako.

Ukubwa wa Vifaa Humaanisha Utendaji Bora Zaidi

Kwa kiasi flani stori hii ina ukweli, lakini ukweli ni kwamba sio kiashiria cha kutosha cha utendaji. Kuna simu nyingi za Android zinazotoka kila mwaka, na baadhi yake zina vifaa vya kushangaza. Hata hivyo, kuwa na vifaa vizuri ndani yake haimaanishi simu nzuri.

Kamera za simu za mkononi ni wahusika wakuu wa vita hii ya vifaa bora. Ukweli ni kwamba, kamera ya megapixel 12 inaweza kuwa chini sana kiuwezo kwa kamera ya megapixel 8 katika kila aina ya kipengele isipokuwa ukubwa wa picha.

Kwa kuongeza, kuna mambo mengine yanayohusika. Kwa mfano, kuna simu nyingi za Android zilizo na specs bora zaidi kuliko iPhone, lakini hiyo haimaanishi kuwa simu ni bora zaidi au inafanya kazi haraka kuliko ile iliyo sifa za kawaida. Masuala ya mfumo wa uendeshaji yanahusika, kama ilivyo kwa tabia ya mtumiaji wakati wa kuitumia.

Sifa za sifu (specs) ni kwa wauzaji kuwashawishi watumiaji kununua; usidanganyike.

Chaja Pekee Unayopaswa Kutumia ni Ile Iliyokuja na Simu yako

Kwa kiasi fulani, hadithi hii ipo tu kwajili ya kunufaisha mifuko ya mtengenezaji wa simu. Wakati simu za mkononi zina faida ndogo, soko la vifaa vya simu hongeza zaidi mapato ya kampuni.

Ukweli wa suala hilo ni kwamba chaja yoyote inayoendana na chaja halisi ya simu yako ni salama kutumia kwenye simu yako.

Kitu ambacho watumiaji wengi hawaelewi ni kwamba kuna tofauti kati ya chaja ya kisasa kutoka kwa kampuni nyingine, na chaja za Kichina za bei nafuu. Wazalishaji bora, kama vile Belkin, Amazon na wengine ni salama kabisa kutumia kwenye simu janja yako, kwa sababu zimetengenezwa kwa kuwa na sifa sawa na chaja orijino za Apple.

Kutumia chaji za kichina, kwa upande mwingine, ni hatari zaidi.

Kuchaji Simu Yako Usiku Mzima Unaua Betri

Hii ni hadithi nyingine ambayo kipindi flani ilikuwa ya kweli, kwa kuwa teknolojia za betri na chaja zimebadilika, stori hii sasa ni uongo kabisa. Betri za zamani hazikuwa na uwezo wa kutosha wa kutambua zinapokuwa zimejaa kabisa, na kuendelea kuzichaji (overcharging) mara kwa mara ilisababisha kupungua kwa maisha ya betri.

Mfumo wa kuchaji wa leo ni nadhifu. Mara tu baada ya simu yako kujaa kikamilifu, inaacha kupokea umeme.

Inakubalika kabisa kuchaji simu janja yako wakati umelala.

Watumiaji Wanapenda Simu Ndogo

Tulikua tunaelekea mwelekeo huo. Lakini hatuko huko tena.

Tabia ya watumiaji imebadilika, kuna kipindi simu zenye umbo dogo zilitawala kila mahali, skrini za sasa ni kubwa zaidi kuliko hapo awali. Inaonekana, watumiaji wanapenda sana simu kubwa ambazo wanaweza kutumia apps za majengo, barua pepe, game na majadiliano ya video kwa urahisi zaidi. Mafanikio ya iPhone 6 Plus na Galaxy Note yanatupa ushahidi pekee unaohitajika kuonyesha kwamba mahitaji ya walaji yameanza kuhama na kuelekea kupenda simu kubwa na zenye nguvu zaidi.

Hii ndio sababu imeibuka sehemu ndogo ya simu za mkononi inayojulikana kama “phablet” ili kusaidia kukidhi mahitaji haya. Hii inakuwa upande mmoja Simu na upande mwingine, tablet na bila shaka siku za usoni itakuwa sehemu kubwa ya soko la simu za mkononi .

Kuzima Simu / Kuondoa SIM / Kuiweka Airplane Mode Inazuia Kufuatiliwa

Kwanza, hebu tuzungumzie airplane mode. Kuweka simu yako katika airplane mode kimsingi inazima Wi-Fi na huduma ya simu za mkononi ili kuwa kama “do not disturb” ya simu yako. Hii haitamzuia mtu yeyote kukufuatilia, hasa kupitia satelaiti.

Unajua, kimsingi  simu ina mifumo miwili ya uendeshaji. Ya kwanza inakuuunganisha na mitandao ya simu za mkononi iliyo karibu nawe wakati nyiingine ni interface ya moja kwa moja kati ya simu na watumiaji. Unapoiweka simu yako katika airplane mode, inazima sehemu moja ya mfumo wa uendeshaji (anaotumia mtumiaji), lakini sehemu ya simu yako inayowasiliana na mitandao ya simu bado inafanya kazi. Haitazuia wewe kufatiliwa.

Ukweli ni, simu inahitaji nguvu ili kutransmit signal, hivyo kuzima simu, au kuondosha betri ni kweli itazuia wewe kufuatiliwa (au unaweza kutumia burner phone). Isipokuwa, sio kila wakati. Simu zilizoathiriwa na aina fulani za programu zisizofaa (malware), kama vile 10,000 wanaokadiriwa sasa wanaendesha PowerOffHijack ya Android (hapana, huwezi kuipata kwenye Google Play) husababisha uone kama simu tayari imezima wakati kihalisia bado haijazima, na inawezekana wanakufuatilia wewe.

Njia pekee ya kuepuka kufuatiliwa ni kuondoa betri. Bila shaka, ikiwa unatumia iPhone 6, Galaxy S6, au simu nyingine ambayo haukuruhusu kutoa betri, chaguo pekee kuacha kutumia simu hiyo ikiwa unahisi unafatiliwa.

Mipangilio ya Brightness ya moja kwa moja Inahifadhi Betri

Huu ni uongo kabisa. Wazo ni, kwa kutumia light sensor iliyo ndani ya simu janja yako, inaweza moja kwa moja kuweka mwanga sahihi ili kuokoa nguvu ya betri.

Ukweli ni kwamba, hii inaweza kuokoa nguvu kidogo ya betri kwa kupunguza mwanga wa skrini inapohitajika, lakini light sensor inatumia nguvu zaidi kwajili ya kutuma taarifa kwenye CPU yako ili kufanyia kazi data ilizokusanya na kuamua mwanga mdogo ama mkubwa upi ni sahihi kwa wakati huo.

Hali ya Android kuwa Open Source Hufanya iwe Rahisi Zaidi Kuvamiwa

Programu ya chanzo cha wazi (Open source software) kwa ufafanuzi wake, mzuri, zipo wazi. Kutoa upatikanaji wa utendaji wa ndani wa mfumo wa uendeshaji inaweza kusababisha vikwazo, lakini unaweza kushangaa kujua kwamba Android kama mfumo wa uendeshaji ni salama sana.

Kitu ambacho sio salama ni apps. Hali ya wazi ya sokoni la programu, na uwezo wa kutumia programu zinazotoka nje ya sehemu kuu ya soko la Google Play hufanya simu za Android ziwe kwenye hatari zaidi ya kuathiriwa na matumizi mabaya kuliko Apple kwa sababu ya app store yake  yenye nguvu sana.

Je! Kuna dhana/stori yoyote ungependa kuongeza? Tuambie kupitia sehemu ya maoni hapa chini na tujulishe ni stori gani ya simu za mkononi ambayo ungependa kuona inapotea.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA