Sambaza:

Baada ya maandamano ya wasanii wa Filamu nchini, Bongo Movie, ambao wameandamana jana katika mtaa wa Aggrey Kariakoo wakipinga uingizwaji wa filamu za nje kwa kudhoofisha wa filamu za ndani, msanii wa tasnia hiyo Steve Mengele Nyerere amefunguka kuhusu tukio hilo.

Steve ameeleza sababu za yeye kutokuungana na wasanii wenzake:

“Binafsi ninalipinga hili, wasanii tunataka kutumika ndivyo sivyo, siwezi tu kuambiwa kuwa kuna maandamano nikaenda.

“Tunavyosema filamu za nje zinazuia soko la ndani ni uongo, hizi filamu za nje tangu tunazaliwa zilikuwepo, tumewakuta akina Arnold Schwartzneger na Rambo, filamu zao zilikuwa zinauzwa Kariakoo. Tulichukua majority yao tukatengeneza filamu zetu. Tuliwakuta Nigeria tukashindana nao tuaweza, hata za filamu za Kihindi tuliweza kushindana nazo.

“Hatujawahi kumzuia Yemi Alade afanye muziki hapa nchini ijapokuwa tuna wanamuziki wetu akina Diamond na Ali Kiba.

“Nachoweza kusema ni kwamba turudi tuangalie ni wapi tumeharibu, tuache kuingiza visingizio ambavyo havina mantiki. Wafanyabiashara Kariakoo wanauza filamu zinazouza na siyo uzalendo.

“Watanzania tumezoea kukaa mezani na siyo kufanya maandamano. Utazuia Dar, je vipi kuhusu Arusha, Dodoma, Mwanza na kwingine?… Hili janga sio la Dar es Salaam pekee ni la Tanzania nzima.

“Mpaka sasa msambazaji ni mmoja, kalemewa mzigo, serikali iruhusu wasamazaji wengine waingine kwenye biashara hii.”

“Tumeshindwa kutengeneza ladha ya Watanzania, tusiwaadhibu wafanyabiashara, tujiadhibu sisi wenyewe kwa kutengeneza filamu zisizouza.” Alisema Steve Nyerere.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako