Nyingine

Squeezer- Wasanii wa sasa wanatunga nyimbo zenye ladha ya ‘bubble gum’

Msanii mkongwe kwenye game ya bongofleva, Squeezer ameongea kuhusu muziki unaofanywa na wasanii wengi wa sasa kwamba hauwezi kudumu kwani wengi wanaokimbilia kufanya sanaa hiyo hawana ubunifu wa kutosha.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio muimbaji huyo amedai nyimbo nyingi za vijana wa sasa zikisikilizwa mara kwa mara zinakera masikio ya watu.

“Nyimbo pamoja na wasanii wengi wa sasa wapo mbioni kupotea kutokana na kuwa na ubunifu mdogo sana katika kazi zao, wengi hawana ‘knowledge’ ya kutosha. Wanatunga nyimbo zenye ladha ya ‘bubble gum’ mtaani wanaziita hivyo kwa kuwa haziwezi kudumu zaidi ya miezi miwili. na nyie watangazaji mnavyozipa muda hewani ndo zinakuwa hata mwezi haziwezi kusurvive”.

Squeezer pia amewashauri wasanii warudi shule ili kupata uelewa katika kuboresha kazi zao na kusisitiza kwamba kama ni muziki upo kila siku na siku zinavyozidi kwenda hela zinazidi kuwa nyingi na kunamuongezea heshima msanii.

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close