SportPesa yatoa elimu kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kwa wanamichezo


Wachezaji wa Singida United siku ya jana wakiongozwa na kocha mkuu Hans Van der Pluijm walipata fursa ya kutembelea ofisi za kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ambao ni wadhamini wao wakuu kwa ajili ya kuweza kufahamiana na kubadilishana mawazo.

Moja ya shughuli ambazo ziliweza kufanyika wakati wa uwepo wao kwenye ofisi hizo ni pamoja na somo kwa wachezaji na viongozi kutoka kwa Meneja Mkuu wa Masoko, Kelvin Twissa lililojikita katika matumizi ya mitandao ya kijamii sambamba na kwa wachezaji kujiongezea thamani na kutengeneza nembo zao kibiashara kupitia majina yao.

SOMA NA HII:  Vanessa Mdee amezindua ‘app’ ya simu ya Vee Money

Sportpesa imewashauri wachezaji kujiongeza kwa kuwaonesha mashabiki wao vitu vyao binafsi kama video na picha wakiwa kwenye mazoezi na kujibu baadhi ya maoni ya mashabiki wao.

matumizi ya mitandao ya kijamii
Wachezaji wa Singida United wakifuatilia somo kwa ukaribu zaidi

Mbali na hayo SportPesa pia wameelezea faida za mchezaji wa mpira wa miguu kujitangaza kuwa itamsaidia kutafutwa na makampuni makubwa ya vifaa vya michezo yeye kama yeye. Mfano Nike, Reebok, Puma n.k

Singida United itakuwa ni timu ya pili kutembelea ofisi za SportPesa baada ya Simba SC kufanya hivyo Alhamisi ya wiki iliyopita ya Oktoba 12 kwa lengo hilo hilo la kufahamiana sambamba na kubadilishana mawazo.

SOMA NA HII:  China Kujenga Kiwanda Kikubwa Cha Kutengeneza Vifaa Vya Mawasiliano Tanzania

Je mfumo wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kutoa elimu kwa wanamichezo utasaidi kuongeza thamani ya wachezaji wa Tanzania ?

Niandikie hapo chini sehemu ya maoni, Unazungumziaje mafunzo ya matumizi ya mitandao ya kijamii ? ningependa kusikia kutoka kwako.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA