Apps za SimuIntaneti

SoundCloud inasema “it’s here to stay” richa ya uvumi kuwa imefilisika

Siku za karibuni kumekuwa na taarifa zinazosikitisha kuhusu huduma ya “Ku-Stream” muziki kutoka Berlin, SoundCloud, ambayo wiki iliyopita ilipunguza asilimia 40 ya wafanyakazi wake bila ya onyo.

Mkuu wa kampuni hiyo amejibu tuhuma hizo kwa kusema “SoundCloud is here to stay.” Katika chapisho la blogu lililowekwa kwenye tovuti ya kampuni hiyo , Mkurugenzi Mtendaji Alex Ljung aliwahakikishia watumiaji na wanamuziki kwamba “muziki unaoupenda kwenye SoundCloud hautapotea, muziki ulioshare au ku-upload hauondoki, kwa sababu SoundCloud haifi.”

Mapema wiki hii mtandao wa TechCrunch uliripoti  kwamba, baada ya kufukuza idadi kubwa ya wafanyakazi, SoundCloud bado haina fedha za kutosha na fedha zilizopo zinatosha kuwafikisha mpaka mwanzoni mwa robo ya nne ya mwaka 2017 (karibu siku 80).

Ljung amepingana na kauli hiyo, kwa kusema kampuni hiyo haifi siku za karibuni “Si katika siku 50, si katika siku 80 au wakati wowote ule. Muziki wako ni salama, “aliandika.

SoundCloud haijatoa maelezo zaidi kuhusu fedha zake, lakini stori hii imezidi kuwa na uzito kutokana na mwanamuziki kutoka Marekani Chance The Rapper, ambaye alianza kufanikiwa kimuziki kupitia SoundCloud.

Wiki iliyopita alionekana kama ameingia kwenye mazungumzo na SoundCloud,bado haijajulikana kama alitoa ushauri ama msaada wa kifedha.

Baada ya majadiliano na Ljung, Chance aliandika kupitia twitter, “Just had a very fruitful call with Alex Ljung. @SoundCloud is here to stay.”

SOMA NA HII:  Messenger Kids: Wazazi sasa wanaweza kuwaruhusu watoto wao kujiunga na Facebook

Haijulikani kama mwanamuziki huyo amefanya uwekezaji kwenye kampuni hiyo au ametoa aina nyingine ya msaada. “Kama mwanachama mwenye nguvu wa jamii ya SoundCloud, Chance The Rapper  ameungana na  mwanzilishi na mkurugenzi Mtendaji, Alex Ljung, kuzungumzia uvumi na taarifa zinazovumishwa,” msemaji wa kampuni aliiambia TechCrunch.

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako