Nyingine

Soma Alichoandika Rais wa TFF, Jamal Malinzi Kuhusu Uwanja Wa CCM Kirumba- Mwanza

Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania, Jamal Malinzi ametoa taarifa nzuri kuhusu uwanja wa CCM Kirumba na wana Mwanza.

Kwa mujibu wa Malinzi, uwanja wa CCM Kirumba sasa unaweza tumika kwa mechi za kimataifa baada ya wataalamu wa Ufundi wa CAF kwenda Mwanza kuukagua uwanja huo mwishoni mwa mwaka jana.

Viwanja vingine ambavyo CAF na FIFA inavitambua nchini hadi sasa ni Amani wa Unguja, Zanzibar, Azam Complex na uwanja wa taifa wa Dar es Salaam.

“Wana Mwanza hongereni Uwanja wa CCM Kirumba umepitishwa na CAF na FIFA kutumiwa kwa mechi za Kimataifa.”

Kupitishwa kwa CCM Kirumba kuna maana kuwa sasa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA ruksa kufanyika huko.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Tecno S1 na Bei yake Nchini Tanzania

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako