Sambaza:

Kurudi kwa simu zenye skrini mbili hakujaja kutoka kwenye kampuni zilizotarajiwa kufanya hivyo, badala yake, imetoka kwa ZTE.

Baadhi yetu sasa hivi:
skrini mbili

Na wengine:

ZTE, imezindua Axon M, smartphone ambayo ina skrini mbili – hii sio simu ya kwanza yenye skrini mbili, lakini hii ndiyo simu ya kwanza yenye skrini mbili ambayo kwa kweli inamuonekano mzuri.

Ya kwanza ilikuwa Kyocera echo :

Ufafanuzi-zaidi, ina skrini mbili za HD 5.2 inch- hii itakuwezesha kuibadilisha kutoka kuwa simu ya kawaida na kuwa tablet ndogo ya inchi 6.7. Pia ina Snapdragon 821 SoC na 4GB ya RAM.  Simu hii inatumia Android 7.1.2 Nougat na kuna kamera moja ya 20MP, pia ina speaker mbili, audio jack 3.5mm , na betri ya 3180mAh.

SOMA NA HII:  Tecno Camon C8 vs Tecno Boom J8 – Ninunue simu gani ?

skrini mbili- mediahuru

Je! ina maana gani kuwa na simu yenye skrini mbili kama hii?

Naam, unaweza kufungua programu tofauti kwenye kila kionyesho (display) – kwa mfano, kuangalia video kamili kwenye skrini moja na kuandika vitu kwenye skrini nyingine kwa wakati mmoja.

Hata hivyo, nina wasiwasi, kwa sababu, skrini mbili ina maana kwamba matumizi makubwa zaidi ya betri. Pia usisahau kuhusu ukweli kwamba hii haiwezi kudumu kutokana na kwamba mbele na nyuma ya simu kumetengenezwa na kioo, pamoja na ulinzi wa kioo wa Gorilla Glass 5.

Kama siku zote, Ningependa kujua nini unachofikiria juu ya hii simu – ni nzuri ama haifai?

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

This article has 2 comments

  1. Julius Reply

    ZTE wamerudisha mfumo wa simu ambao umepotea kwa miaka mingi ni wazo zuri ila naona hii simu haitafaa kwa matumizi ya watuwengi

  2. Amani Reply

    Kwa kweli ZTE wamejitahidi kwa kuja na toelo hili jipya. Ila wasiwasi wangu mkubwa ni kwenye skrini ya pili inaweza kutofanya kazi kwa jiali ya kufungua mara kwa mara.
    Pia sijapenda upigaiji wake wa picha kwani kamera iko moja ila inabidi ubadili skrini kama unataka kuiga picha kawaida na sio Selfie

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako