Unaweza kupata maoni tofauti kuhusu simu za Tecno nchini Tanzania. Baadhi ni sifa nzuri sana wakati sifa zingine ni mbaya kabisa. Wakati huo huo kuongezeka kwa mauzo ya simu za Tecno nchini Tanzania kunathibitisha kuwa brand ya Tecno tayari ina msingi wa watumiaji waaminifu na msingi huu unaongezeka kwa kasi.

simu-za-tecno-nchini-tanzania

Wakati watu wengine wanasema Tecno ni tu kelele, ni PR tu lakini hamna kitu – tunaamini brand hii ipo hapa kukaa nasi kwa miaka mingi zaidi – Tecno ina uwezo mkubwa wa kutawala soko la simu janja nchini Tanzania na kushindana na bidhaa kubwa kama Samsung.

Hizi ni sababu kuu kwa nini Tecno inafanya vizuri sana nchini Tanzania.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno WX4 na WX3 bei na Sifa zake

simu za Tecno
1. Bei ya chini ya simu za Tecno

Katika nchi kama Tanzania – bei ni jambo kubwa. Kwa kipaumbele hicho cha bei ya chini kinafanya tecno kuwa na nguvu kubwa kwenye mauzo ya bidhaa zake.

2. Ubora wa vifaa vya Tecno

Unaweza kuishtaki Tecno kwa kuwa ya Kichina, lakini huwezi kuwashtaki kwa kuwa na ubora duni. Bidhaa zao hufanya kazi vizuri na ni za bei nafuu. Simu za Tecno zinaweza kuwa na uwezo sawa na simu za Samsung, lakini mara nyingi – kwa nusu ya bei.

Mbali na hilo – ubora wa bidhaa huhakikisha uaminifu wa watumiaji. Kuna watanzania wengi ambao walikuwa wakitumia vifaa vya Tecno vya bei ya chini (uwezo) kabla na walifurahia ubora wake. Muda wa kuingia kwenye utumiaji wa simu janja ulipofika – wamechagua Tecno tena .

SOMA NA HII:  Jinsi ya kuficha (hide) picha kwenye simu za android

3. Soko Sahihi

Tecno inaendesha kampeni za kuvutia za masoko ambazo zinalenga wateja wao wa msingi.
Wanaelewa nani ni mteja wao na kujaribu kuwa pale ambapo mteja wao yupo. Badala ya kutoa simu za bure kwajili ya mapitio/uchambuzi kwenye blogu, wao wanazingatia wauzaji, wafanyabiashara wa simu – wakubwa na wadogo, badala ya kupoteza muda na pesa kwenye techies muhimu – watu muhimu kwa jamii. Kwa sababu wanajua kwamba sehemu kubwa ya wateja wao hawasomi blogu kama Teknokona na tovuti zingine kama hiyo

4. Ubunifu mnzuri

Ingawa simu za Tecno ni za bei nafuu – hazionekani kama za bei nafuu. Ubunifu ni mzuri sana na baadhi ya matoleo ya Tecno yana mtazamo wa kifahari.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno W4 bei na Sifa zake

Zaidi kuhusu simu za Tecno nchini Tanzania:

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

This article has 1 comment

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako