Sambaza:

Simu za mkononi zimekuwa kitu cha kawaida barani Afrika. Kwa vijana wengi, simu ni kifaa cha kawaida hivi sasa. Wanafunzi wengi zaidi wana uwezo wa kutumia simu janja ambazo zinaweza kuunganishwa kwenye mtandao – na wanaenda nazo shule.

Simu za mkononi mara nyingi wanazitumia shuleni haijarishi wanaruhusiwa au la. Ingawa zina wawezesha kupata habari muhimu, pia huleta majukumu mapya na hatari. Hivi sasa inaanza kuwa kawaida kwa kipindi kuingiliwa na simu ya mwanafunzi au mwalimu. Upatikanaji wa ponografia pamoja na uonevu na unyanyasaji kwa njia ya simu unaripotiwa mara nyingi.

Simu za mkononi zimechukua nafasi kubwa katika maisha ya vijana wengi. Kabla ya simu ya mkononi kuwasili Afrika, watu wachache walikuwa wanatumia simu za mezani. Simu ya mkononi inawakilisha mapinduzi makubwa ya mawasiliano barani Afrika kuliko mabara mengine.

SOMA NA HII:  Orodha ya Maneno ya Teknolojia na Tafsiri zake kwa Kiswahili

Matumizi ya simu ya mkononi ni ya juu zaidi kuliko takwimu za umiliki zinavyo onyesha.

Mara nyingi wanafunzi huazimana simu, wengine wanaazima kwa wazazi wao, ndugu wengine wa familia na kwa majirani.

Wanafunzi wachache hutumia simu zao kutembelea tovuti mbalimbali kwa lengo la kupata msaada wa kimasomo . Lakini faida huonekana kuwa ni ndogo kwa matumizi mengine ya kawaida kama vile kuwasiliana na marafiki kujua habari za wimbo ama movie mpya au kutumia simu kama calculator. Matumizi mengi ya simu za mkononi kwa wanafunzi si salama: utendaji wa kitaaluma unaathiriwa na matumizi mabaya ya teknolojia – kulala darasani kwa sababu ya kupiga simu za bei nafuu usiku, kupoteza muda mrefu kwenye tovuti za mitandao ya kijamii, na ponografia.

Walimu nao wanatumia simu wakati wa vipindi. Serikali na mashirika mbalimbali ya kijamii inabidi kufanya kazi kukuza matumizi bora na sahihi ya simu za mkononi shuleni.

Tunapenda kusoma maoni yako, tuambie una maoni gani ? Je una suluhisho thabiti la kukuza matumizi bora na sahihi ya simu za mkononi shuleni.

 

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako