Simu za Mkononi

Listi ya Simu 5 za Halotel zinazouzwa kwa bei nafuu kabisa.

Halotel ni jina la kibiashara la kampuni ya Viettel Tanzania Ltd, mwanachama wa Viettel Group. Viettel ni kampuni kubwa ya mawasiliano nchini Vietnam, mapato yake kwa mwaka 2015 ni karibu dola bilioni 11.

Mbali na Vietnam, Viettel imewekeza katika sekta ya mawasiliano katika nchi 10 katika mabara matatu, ikiwa ni pamoja na; Cambodia, Laos, Timor Leste, Myanma kwa Asia, Msumbiji, Cameroon, Burundi, Tanzania kwa Afrika na Haiti, Peru kwa Amerika. Ilizinduliwa rasmi tarehe 15 Oktoba 2015, na kutoa huduma zake za simu katika maduka 30 nchini nzima .

Halotel inasifika kwa uwezo wake wa kufika maeneo mengi Tanzania ndani ya muda mfupi tangu kuanzishwa kwake hasa katika maeneo ya vijijini.

Leo hatutazungumzia sana historia ya Halotel na uwezo wake kwa sababu makala hii inahusu simu za halotel zinazouzwa kwa bei nafuu kabisa. Imezoeleka kwa mitandao ya simu Tanzania kuuza simu zenye nembo zao kwa bei nafuu huku zikiwa na ofa nyingi kwa wanunuzi wa simu hizo.

Hii ni listi ya simu za halotel kali na za kijanja mpya kabisa unazoweza kununua kwa bei nafuu:

Simu za Mtandao wa 2G

Halotel H6402

Simu ya halotel H6402 ni simu nzuri kwa wale wanaopenda simu yenye uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu, zinatumia laini mbili ila laini ya kwanza lazima iwe halotel na laini ya pili yoyote inafanya kazi.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Itel S12 bei na Sifa zake

Simu hii ina kioo chenye inchi 2.4, Tochi, Bluetooth, MP3, FM, GPRS na betri yenye ujazo wa 1400 mAh. Mwanzo simu hii ilikuwa inauzwa Tsh 49,000 lakini sasa inauzwa Tsh 26,000.

Halotel H6307

Uwezo wa Simu hii ni mzuri kwa mtu yeyote anayetaka simu ya bei nafuu kwani simu hii ina uwezo wa kutumia laini mbili, ina kioo chenye inchi 1.77′ , Bluetooth, MP3/MP4, FM, betri yenye ujazo wa 1000 mAh, kamera yenye 0.08 MPx na memori ya ROM ya ukubwa wa 4 GB. Mwanzo simu hii ilikuwa inauzwa Tsh 26,000 lakini sasa inauzwa Tsh 22,000 tu.

Halotel H6308

Simu hii haijapishana sana na simu ya H6307 kwani simu nayo ina uwezo wa kutumia laini mbili, ina kioo chenye inchi 1.77 , Bluetooth, MP3/MP4, FM, betri yenye ujazo wa 1000 mAh, kamera yenye 0.08 MPx na memori ya ROM ya ukubwa wa 4 GB. Mwanzo simu hii ilikuwa inauzwa Tsh 26,000 lakini sasa inauzwa Tsh 22,000 tu.

Halotel H6309

Simu hii inafanana na simu ya H6307 kwani simu nayo ina uwezo wa kutumia laini mbili, ina kioo chenye inchi 1.77 , Bluetooth, MP3/MP4, FM, betri yenye ujazo wa 1000 mAh, kamera yenye 0.08 MPx na memori ya ROM ya ukubwa wa 4 GB. Mwanzo simu hii ilikuwa inauzwa Tsh 26,000 lakini sasa inauzwa Tsh 22,000 tu.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Huawei Nova 2S Bei na Sifa Zake

Samsung Galaxy J1

Simu hii ni toleo maalumu kwajili ya Halotel hivyo lazima utumie laini ya halotel na laini nyingine, tofauti na Samsung Galaxy J1 ya kawaida.

Uwezo wa Simu

  • Dual SIM
  • Mtandao: GSM, HSPA, LTE
  • Chip: Spreadtrum Dual-core 1.2 GHz
  • Upana wa Kioo: 4.3” WVGA 400×800 pixels
  • Memori: 4 GB ROM + 512 MB RAM
  • Kamera: 5MP AF + 2.0MP FF
  • 1850mAh Betri

Bei ya simu hii kwenye maduka ya halotel ni Tsh 260,000.

Kuna simu nyingi zinazouzwa na mtandao wa simu wa halotel hapo juu ni baadhi ya simu za bei nafuu kabisa ambazo watazania wengi wanaweza kununua. Kuangalia list ya simu zingine zinazouzwa na Halotel tembelea tovuti yao kwa kubonyeza hapa.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako