Ifahamu simu ya Vodafone Smart Kicka 2 kutoka Vodacom #Uchambuzi


Simu za kisasa za smartphones kutoka makampuni makubwa kama vile Apple, Sony na Samsung ni ghali sana kwa watu wengi wa Tanzania. Au watu wengine ambao hawataki kuvunja benki kwajili ya simu.

Simu ya Vodacom Smart Kicka ya mwaka 2014, ambayo ilikuwa na gharama ya Sh 79,999 tu, ilionekana kuwa bora. Siyo tu ilitolewa ikiwa na vipengele vizuri na vya kutosha kwa wengi, lakini ilifanya hivyo kwa bei ambayo ilikuwa rahisi kwa watu wengi.

Imepita miaka mitatu tangu uzinduzi wa Smart Kicka ya kwanza, na ni wakati wa kuboresha zaidi kifaa hiki- bei pia imepungua zaidi na sasa ni Tsh 60000.

Katika uchambuzi huu, sitajaribu kulinganisha Smart Kicka 2 na smartphones nyingine za gharama kubwa. Hiyo haitakuwa haki. Badala yake, lengo langu ni kuonyesha nguvu iliyowekwa na Vodacom katika kutengeneza kifaa hiki cha bei nafuu, nguvu kubwa sana ambayo haipaswi kubezwa.

Nini kimebadilika

Mbali na mwonekano mpya, Smart Kicka 2 mpya sasa inakuja ikiwa tayari imewekwa Android 5.1 Lollipop na inatumia “quad-core processor” badala ya  “dual-core” inayotumika kwenye toleo la kwanza.

smart-kicka-2-kutoka-vodacom

Smart kicka 2 ina kioo cha rangi inchi 3.5, hifadhi ya ndani ya 4GB  na betri ya 400mAh . Kama toleo la kwanza, uwezo wa kuhifadhi unaweza kupanuliwa hadi 32GB na kadi ya hiari ya microSD, Smart Kicka 2 ina kamera ya 2.0 megapixel kwa nyuma na 512MB tu ya RAM.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Huawei Nova 2S Bei na Sifa Zake

Licha ya bei yake ya chini, Smart Kicka 2 huunganisha kwa urahisi mitandao ya Wi-Fi na inaweza hata kuunganishwa na vifaa vya Bluetooth. Haina GPS au 4G / LTE inatumia 3G na inakuja na “stereo headphone” ambazo wakati mwingine hutumiwa kama antenna ya redio ya FM.

Vipengele Bora Zaidi

Smart Kicka 2 inajumuisha mwongozo wa moja kwa moja. Inakuonyesha jinsi ya kuandaa kifaa chako kwajili ya  matumizi katika hatua chache tu, kama kuingiza betri na kadi ya Sim. Navigation ya msingi ya Android pia imefafanuliwa.

Vodacom ina “Android skin” yake na programu yake ya app store . Wakati wa matumizi ya mara ya kwanza, vidokezo vingi na msaada hutolewa kwenye skrini kuhakikisha watumiaji wanajua jinsi ya kutumia zaidi simu zao. Vodacom imejaribu vizuri kabisa kuweka installation, usanidi na matumizi ya kila siku kuwa rahisi na yanayoeleweka.

Smart Kicka 2 inakuja ikiwa tayari imewekwa apps za Google, ikiwa ni pamoja na YouTube, Chrome, Gmail na Google Maps, pamoja na programu za mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter. Vodacom app store inakuwezesha kuvinjari na kufikia maudhui mengi ya Tanzania, kuangalia salio na kununua muda wa maongezi au vifurushi.

SOMA NA HII:  Vodacom Yasitisha Huduma za Kununua Umeme za Luku

Kuongeza ofa zaidi, simu inakuja na muda wa maongezi wa dakika 1200, sms 10000 na 1GB ambazo unapaswa kuzitumia ndani ya mwezi mmoja.

Hisia nzuri

Haitashangaa kwamba kwa bei hii ya chini, Smart Kicka 2 ni kifaa kilichoundwa kwa plastiki. Kwanza ni nyepesi, imetengenezwa vizuri. Ukubwa wake ni mzuri ikiwa mkononi.

Kutokana na ukweli kwamba watu wengi wanatumia mkono wa kulia, kwa hiyo watatumia kitufe cha kulia kufanya kazi na kuvinjari kwenye simu zao, Vodacom ilichagua kuweka kitufe chake kwenye upande wa kulia wa simu hii.

Scrini na kamera

Screen resolution ya saizi za 320 × 480 haijabadilika kutoka kwa Smart Kicka ya kwanza. Hebu tuseme nayo: kwa skrini tu ya kipenyo cha 3,5-inch, nani anahitaji pixels zaidi? Mwangaza wa skrini (Screen brightness) ungekuwa bora zaidi, ingawa: si rahisi kusoma kwenye jua la moja kwa moja.

Ubora wa scrini sio wa kuridhisha sana lakini kwa kuzingatia kiwango cha chini cha bei, ubora wa skrini ni bora zaidi na unatosha.

smart-kicka-2-kutoka-vodacom
Picha iliyochukuliwa kwa kutumia Smart Kicka 2

Smart Kicka ina kamera moja tu kwa nyuma, ambayo inatosha kwa watu wengi ambao wanataka tu kupiga picha mara kwa mara na hawana haja ya picha za ubora wa juu. Kwa hiyo, kamera ya megapixel 2 inafanya kazi nzuri.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Infinix Zero 5 bei na Sifa zake

Vifaa na utendaji

Wakati Smart Kicka ya 2014 ilikuwa na dual-core processor , Kicka 2 sasa ina cores nne. Matokeo yake ni kuwa smartphone ambayo hutoa urambazaji laini (smooth navigation) na uendeshaji wa operesheni za jumla. Usitarajie kucheza michezo “games” ya kisasa kwenye simu hii.

Ukosefu wa nguvu halisi ya kuendesha simu unaonekana dhahiri katika hali ambayo vitu vingi vimefunguliwa kwenye skrini, kama vile wakati wa kuchukua picha. Kutokana na bei ya Kicka 2, tena bado hakuna vitu vingi ambavyo unaweza kuvilalamikia.

Uhai wa betri

Ikiwa na betri yake ya 400mAh, Smart Kicka 2 itakaa siku moja ikiwa huitumii mara kwa mara kuvinjari mtandao au kuchukua picha.

Hitimisho

Smart Kicka 2 ya Vodacom bila shaka ni mpango mzuri kama mtangulizi wake. Ingawa maboresho ni madogo – mchakato bora, toleo jipya la Android na muundo bora zaidi – hutoa kila unachohitaji, na zaidi, kutoka kwenye simu ya smartphone inayo gharama Tsh60000 tu.

Vodacom Smart Kicka 2 inapatikana kwenye maduka yote ya Vodacom hivi sasa. Inapata 8/10. – © 2017 Mediahuru

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA