Ifahamu simu ya Tecno W2 bei na Sifa zake


Unaweza kuichukulia simu janja ya Tecno W2 kama simu ambayo ni entry level kutoka Tecno kwa mwaka wa mwaka 2016. Ni simu ya bei nafuu iliyozinduliwa na Tecno mnamo 2016. Tecno W2 ina skrini ya ukubwa wa 4.5-inch na kamera ya nyuma ya 2MP.

Sifa Muhimu za Tecno W2

  • Kioo: 4.5-inch Touch Display, 480 x 854 pixels (217ppi)
  • Processor: 1.3GHz quad-core
  • Uwezo wa RAM: 1GB RAM
  • Mfumo wa Uendeshaji: Android 6.0 (Marshmallow)
  • Hifadhi ya ndani: 8GB
  • Hifadhi ya Ziada: Unaweza kuweka memori kadi hadi ya 32GB
  • Kamera ya Nyuma: 2MP
  • Kamera ya Mbele: 0.3MP
  • Dual-SIM, Micro-SIM
  • Uwezo wa Betri: 2500 mAh

Sifa Zingine

Kila kitu kuhusu Tecno W2 ni cha kawaida. Ni simu janja kwa ajili ya watu wanaopenda simu za bei nafuu. Kioo chake kina 4.5-inch na resolution ya 480 x 854 pixels. Tecno W2 ina megapixels 2 kwenye kamera ya nyuma, mbele ina kamera ya 0.3 megapixel..

Tecno W2 inakuja na Android 6.0 (Marshmallow) kwenye 1.3GHz quad-core processor na RAM 1GB. Ina 8GB ya hifadhi ya ndani, lakini unaweza kuongeza kadi ya kumbukumbu hadi 32GB. Tecno W2 ina betri ya 2500 mAh.

Bei na Upatikanaji

Tecno W2 inapatikana nchini Tanzania, Nigeria na Kenya. Unaweza kununua simu hii katika maduka ya mtandaoni katika nchi husika. Bei ya Tecno W2 nchini Tanzania inatofautiana kati ya Tsh 110,000 hadi Tsh 150,000.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA