Ifahamu simu ya Tecno i5 Pro bei na Sifa zake


Simu ya Tecno i5 Pro ni toleo ambalo ni maboresho ya simu janja ya i5. Kwa bei ndogo, inakupa RAM na hifadhi zaidi, lakini, vipengele vingine, bado vinafanana na simu zingine.

Sifa Muhimu za Tecno i5 Pro

 • Kioo: 5.5-inch IPS Display, 720 x 1280 pixels (267ppi)
 • Processor: 1.5GHz quad-core MediaTek 6737T
 • Uwezo wa RAM: 3GB RAM
 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.0 (Nougat)
 • Hifadhi ya Ndani: 32GB
 • Hifadhi ya Ziada: Unaweza kuweka memory card hadi ya 128GB
 • Kamera ya Nyuma: 13MP
 • Kamera ya Mbele: 8MP
 • Fingerprint Sensor (Mbele)
 • 4G LTE Data
 • Uwezo wa Betri: 4000 mAh

Muonekano na Kioo

Simu janja ya ‘Pro’ ina muundo wa chuma kama toleo la kawaida. Huwezi kungundua tofauti kwa kuangalia tu. Unene, uzito na aina za rangi ni sawa sawa.

Tecno i5 Pro ina kioo cha 5.5-inch na HD resolution ya 1,280 x 720 pixels. Skrini yake ina uwezo mzuri na utafurahia uwezo wa kuonyesha picha vizuri. Rangi zake unapo angalia video ni nzuri sana.

Kamera na Uhifadhi

Kwa nyuma, Tecno i5 Pro ina kamera imara ya megapixel 13. Hii inakamilishwa na sifa kama vile autofocus, subject tracking na flash kwa picha zenye ubora. Pia kuna kamera ya megapixel 8 yenye nguvu kwajili ya selfies na ina LED flash.

Uhifadhi ni kipengele ambapo simu hii imeboresha zaidi ya Tecno i5. Ina hifadhi ya ndani ya GB 32. Unaweza pia kupanua uhifadhi kwa kutumia microSD card hadi ya 128GB.

Utendaji na OS

Quad-core MediaTek MT6737T processor ina tekeleza kazi zote kwenye simu hii. Ingawa inaweza kuonekana kama i5 Pro haiwezi kufanya vizuri zaidi kuliko simu za bei nafuu, GB 3 ya RAM inaonyesha utofauti juu ya uwezo wake. Tecno i5 Pro inakuja na mfumo wa Android 7.0 Nougat, na Tecno HiOS 1.1.

Sifa Nyingine na Uwezo

Inakuja na betri ya 4,000mAh Li-Ion, inakupa masaa mengi ya matumizi kabla ya kuhitaji kuchaji tena. Pia fingerprint scanner inaendelea kukupa nguvu ya ziada ya ulinzi.

Unaweza kufurahia kasi ya kupakua kwenye simu ya mkononi hadi 300 Mbps na 4G LTE. Vipengele vingine vinavyopatikana kwenye Tecno i5 Pro ni pamoja na USB OTG, Bluetooth 4.2, na Wi-Fi 802.11 b / g / n na utendaji wa Wi-Fi na uwezo wa hotspot.

Bei na upatikanaji

Tecno i5 Pro inalenga soko la India na inatarajiwa kwa bei ya INR 12,700 nchini India. Tecno i5 Pro bado haipatikani Tanzania, Nigeria, Ghana, na Kenya na haipatikani hata katika masoko mengine. Ikiwa itaanza kupatikana, unaweza kununua simu hii ya gharama nafuu katika maduka ya mtandaoni nchini Tanzania, Nigeria na Kenya. Bei ya Tecno i5 Pro nchini Tanzania ni kati ya Tsh 442,000 hadi Tsh 662,300 kulingana na eneo ulilopo. Bei nchini Kenya inaanzia karibu KSh 14,499.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA