Ifahamu simu ya Tecno i5 bei na Sifa zake


Tecno i5 ni simu ya mid-range katika simu za i Series inayolenga soko la India. Simu janja hii inakuja na betri yenye uwezo wa juu, kioo kikubwa cha HD, quad-core processor, na RAM nzuri.

Sifa Muhimu za Tecno i5

 • Kioo: 5.5-inch IPS Display, 720 x 1280 pixels (267ppi)
 • Processor: 1.5GHz quad-core MediaTek 6737T
 • Uwezo wa RAM: 2GB RAM
 • Mfumo wa Uendeshaji: Android 7.0 (Nougat)
 • Hifadhi ya Ndani: 16GB
 • Hifadhi ya Ziada: Unaweza kuweka memory card hadi ya 128GB
 • Kamera ya Nyuma: 13MP
 • Kamera ya Mbele: 8MP
 • Fingerprint Sensor (Mbele)
 • 4G LTE Data
 • Uwezo wa Betri: 4000 mAh

Muonekano na Kioo

Simu janja ya Tecno i5 ina muundo wa chuma pia ina wembamba wa 8 mm. Uzito wake ni kama gramu 160. Tecno i5 inakuja katika rangi ya dhahabu, nyeusi na kijivu.

Tecno i5 ina kioo cha 5.5-inch na HD resolution ya 720 x 1280 pixels. Skrini yake ina uwezo mzuri na utafurahia uwezo wa kuonyesha picha vizuri. Rangi zake unapo angalia video ni nzuri sana.

Kamera na Uhifadhi

Kwa nyuma, Tecno i5 ina kamera imara ya megapixel 13. Hii inakamilishwa na sifa kama vile autofocus, subject tracking na flash kwa picha zenye ubora. Pia kuna kamera ya megapixel 8 yenye nguvu kwajili ya selfies na ina LED flash.

Tecno i5 ina hifadhi ya ndani ya GB 16. Unaweza pia kupanua uhifadhi kwa kutumia microSD card hadi ya 128GB.

Utendaji na OS

Quad-core MediaTek MT6737T processor ina tekeleza kazi zote kwenye simu hii. Ingawa inaweza kuonekana kama i5 haiwezi kufanya vizuri zaidi kuliko simu zingine za bei nafuu, GB 2 ya RAM inaonyesha utofauti juu ya uwezo wake. Tecno i5 inakuja na mfumo wa Android 7.0 Nougat, na Tecno HiOS 1.1.

Sifa Nyingine na Uwezo

Inakuja na betri ya 4,000mAh Li-Ion, inakupa masaa mengi ya matumizi kabla ya kuhitaji kuchaji tena. Pia fingerprint scanner inaendelea kukupa nguvu ya ziada ya ulinzi.

Unaweza kufurahia kasi ya kupakua kwenye simu ya mkononi hadi 300 Mbps na 4G LTE. Vipengele vingine vinavyopatikana kwenye Tecno i5 ni pamoja na USB On-the-Go (OTG), Bluetooth 4.2, na Wi-Fi 802.11 b / g / n,  Wi-Fi na uwezo wa hotspot.

Bei na upatikanaji

Tecno i5 inalenga soko la India na inatarajiwa kwa bei ya INR 11,495 nchini India. Tecno i5 bado haipatikani Tanzania, Nigeria, Ghana, na Kenya na haipatikani hata katika masoko mengine. Ikiwa itaanza kupatikana, unaweza kununua simu hii ya gharama nafuu katika maduka ya mtandaoni nchini Tanzania, Nigeria na Kenya. Bei ya Tecno i5 nchini Tanzania ni kati ya Tsh 410,000 hadi Tsh 600,000 kulingana na eneo ulilopo. Bei nchini Kenya inaanzia karibu KSh 14,499.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA