Ifahamu Simu ya Nokia 8 Sirocco Bei na Sifa Zake


Nokia inazidi kujiimarisha kwenye soko la simu za Android kwa kutoa flagship yake mpya kwa mwaka huu na ni simu janja ya Android imara yenye ngumu zaidi duniani. Simu hiyo inayotajwa kuwa ni ngumu kuvunjwa kwa mkono ni Nokia 8 Sirocco. Uzinduzi wa simu janja hii umeleta gumzo kubwa kwa wafuatiliaji wa mambo ya simu.

Kwa mujibu wa kampuni ya HDM Global inayotengeneza simu za Nokia hii ni flagship mpya kwa mashabiki wao ambao wamekuwa wakitafuta simu janja ya kiwango cha juu ambayo ina uwezo wa kufanya kazi zaidi kuliko Nokia 8. Simu janja hii inakuja na vitu tofauti kabisa na tulivyozoea kwenye simu za Nokia.

Muundo wa kava ya simu ya Nokia 8 Sirocco unafanana na ule wa Simu ya Nokia 8800 iliyotoka 2005 ambayo Kava yake ilikuwa imara na ngumu.

Simu ya Nokia 8800 iliyotoka 2005

Muonekano na Kioo

Hii ni tofauti na kitu chochote ulichokiona kutoka Nokia na muundo wake ni wa kisasa sana. Nokia 8 Sirocco ina muundo wa mchanganyiko wa chuma cha pua kilichowekwa kati ya kioo cha Corning Gorilla Glass 5. Pia ni nyembamba sana kwani ina unene wa 7.5mm. Chuma kilichotumiwa kwenye simu janja hii pia ni imara zaidi kuliko flagship zingine ambazo mara nyingi zinatengenezwa na bodi ya muundo wa malighafi ya Aluminium.

Mbali na na kuwa na kava ya chuma pia asilimia 95 ya uso wa nje wa Nokia 8 Sirocco ni kioo. Na kioo chake kimepinda (Curves) kidogo ingawa sio kama kioo kama cha Samsung Galaxy S9. licha ya ugumu wa Bodi yake pia haiingi maji wala kusumbuliwa na vumbi. Ukubwa wa kioo cha simu hii ni 5.5-inch chenye teknolojia ya P-OLED QHD (1440×2560).

Betri na Kamera

High-end flagships kama Nokia 8 Sirocco kawaida huwa hazina betri yenye uwezo mkubwa sana mara zote hubebwa na vipengele vingine. Mbali na hilo, uendeshaji wa betri kwenye simu janja hii ni wa kiufanisi sana. Betri lina ujazo wa 3260 mAh ambapo chaji yake inaweza kukaa kwa siku moja hadi mbili kwa utumiaji wa kawaida pia ina uwezo wa Qi wireless charging.

Mapema HMD ilitangaza ushirikiano na Zeiss-mtaalamu wa optics kutengeneza kamera kwenye simu janja hii. Nokia 8 Sirocco inajiunga na ligi ya viwango cha juu kwa kamera zake mbili za nyuma moja ina ukubwa wa 12MP na nyingine yenye 13MP zikiwa zimetengenezwa na kampuni ya kijerumani ya Zeiss. Kamera ya mbele (Selfie) itakuwa na uwezo wa 5MP na kuweza kurekodi video ya 1080p.

Vifaa na Programu

Kitu kidogo ambacho naona hakipo sawa kwenye Nokia 8 Sirocco ni HMD kutengeneza flagship na chipset ya mwaka jana wakati flagships nyingine tayari zinatumia chipset ya mwaka huu. Ingawa, processor ya Octa-core Qualcomm MSM8998 Snapdragon 835 inayoongozana na Adreno 540 GPU inatoa utendaji wa kuvutia.

Pia, simu janja hii ya Nokia 8 Sirocco inakuja na RAM ya 6GB pamoja na nafasi ya hifadhi ya ndani ya 128GB. Haina uwezo wa kutumia memory card, hata hivyo, 128GB ni nafasi ya kutosha karibu kwa mtu yeyote. Pia inatumia Android 8.0 Oreo.

Bei na Upatikanaji

The Nokia 8 Sirocco was officially announced in the MWC 2018 and would be released in the USA this April. Nokia 8 Sirocco is also scheduled to roll out for a $922 which is about 332, 000 Naira.

Nokia 8 Sirocco ilitangazwa rasmi katika MWC 2018 na itaanza kuuzwa nchini Marekani Aprili hii. Nokia 8 Sirocco inatarajiwa kuanza kuuzwa kwa  $ 922 ambayo ni karibu Tsh 2080,000.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA