Ifahamu simu ya Nokia 7 Plus bei na Sifa zake


Toleo bora zaidi la simu ya Nokia 6 (2018) lilizinduliwa kwenye mkutano wa Mobile World Congresso unaoendelea Barcelona, ​​Hispania. Imepewa jina la Nokia 7 Plus, simu hii ni moja ya simu bora zilizo zinduliwa na kampuni ya simu ya Nokia ikiwa ni pamoja na Nokia 8 Sirocco, Nokia 6 (2018), Nokia 8110 4G na Nokia 1. Nokia 7 Plus ni simu janja ya kati (mid-range smartphone) na pia ina muonekano mzuri. Inakuja na vipengele vingi vilivyoboreshwa ambavyo utavifahamu unavyozidi kusoma makala hii.

simu ya Nokia 7 Plus bei na Sifa zake

Sifa za Nokia 7 Plus

  • Ukubwa Kioo – 6-inch display yenye resolution ya 2,160×1,080
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android Oreo One
  • Uwezo wa Processor – Qualcomm Snapdragon 660 processor
  • Ukubwa wa RAM – 4GB RAM, 64GB storage
  • Uwezo wa Kamera – Ziko mbili moja ina Megapixel 12 na nyingine Megapixel 13 telephoto lens, Kamera ya mbele Megapixel 16
  • Uwezo wa Betri – 3,600mAh non-removable battery with fast charging
  • Bei – Inategemewa kupatikana kwa dollar za marekani $490 sawa na Tsh 1,102,100
  • Upatikanaji – Inategemewa kuanza kupatikana kuanzia Mwezi April mwaka huu 2018.

Kioo na Muonekano

Tofauti na mtangulizi wake , simu hii inakuja na muonekano mpya na ina uwiano wa 18: 9 ambao ni utaratibu mpya kwenye simu janja zinazotoka hivi karibuni. Kwa mujibu wa HMD Global, kwa nyuma imetengenezwa na aluminium. Pia ina fingerprint sensor iliyowekwa upande wa nyuma chini ya kamera.

Nokia 7 Plus inakuja na kioo kikubwa chenye upana wa inchi 6 na resolution ya 2220×1080 ambayo ni sawa na uwiano wa 18:9. Kamera zilizoboreshwa zenye 12-megapixel wide aperture sensor na 13-megapixel kwa upande wa nyuma, pia kamera yenye 16-megapixel kwa mbele.

Betri na Kamera

Ndani ya Nokia 7 Plus kuna betri yenye ujazowa 3, 800mAh. Ingawa hii si betri kubwa, ni kubwa ya kutosha matumizi mazuri kwa siku. Mbali na hilo, pia kuna teknolojia ya kuchaji kwa haraka ya Qualcomm.

Simu hii ina kamera sawa na simu mpya ya Nokia 8 Sirocco. Hii ina maana unapata bothie feature, live bokeh mode, na 2x optical zoom na Zeiss lens. Kuna kamera mbili upande wa nyuma zikiwa na 12MP. Kwa wapenzi wa selfies, Nokia 7 Plus ina 16MP upande wa mbele.

Vifaa na Programu

Nokia 7 Plus inatumia Qualcomm SoC. Octa-core Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 inafanya kazi kwa kasi ya 2.2GHz pamoja na Adreno 512 GPU. Ingawa hii haifanani na yale yaliyotajwa katika simu kubwa kama Samsung Galaxy S9 au LG V30S ThinQ, utendaji wake ni laini sana.

Simu hii inakuja na RAM ya 4GB na hifadhi ya ndani ya 64GB ambayo ni sawa na inayotolewa na Samsung Galaxy S9. Unaweza pia kuongeza hii hadi 256GB ikiwa unataka nafasi zaidi. Inatumia Android Go (Android 8.0 Oreo) ambayo ni mpango wa Google kutoa Android OS ambayo pia inapata sasisho za usalama kutoka kwao.

Bei na Upatikanaji

Nokia 7 Plus ilizinduliwa kwenye MWC 2018 na itakuwa inapatikana kwa ajili ya kuuzwa kuanzia mwezi Aprili kwa karibu dollar za marekani $490 sawa na Tsh 1,102,100.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA