Sambaza:

Infinix Smart X5010 ni ongezeko la kwanza kwenye mfululizo wa “Smart”; aina mpya ya simu janja zenye bei nafuu kutoka Infinix Mobility. Smart X510 ni ni simu janja ya bei nafuu ambayo sifa zake imelenga soko la watu wa chini kabisa. Inakuja na kioo cha HD chenye inchi 5.0, RAM 1GB, hifadhi ya ndani ya 16GB, mfumo wa uendeshaji wa Android 7.0 Nougat na betri ya 3060mAh.

Simu hii inapatikana nchini Tanzania, Nigeria na Kenya kwa bei ya Tsh 180,000. Hapa chini tunazungumzia sifa za Infinix Smart kwa undani zaidi.

Infinix Smart X5010

Sifa na Uwezo wa Infinix Smart (Smart X5010)

Simu ya Infinix Smart  ina kioo chenye inchi – 5.0 , 1GB RAM , 16GB ya hifadhi ya ndani, Android 7.0 Nougat + XOS 2.2 , na betri yenye ujazo wa 3060mAh.

 • Kuzinduliwa : Julai 2017
 • Idadi ya Laini: Laini Mbili
 • 3G Network : HSDPA 850 / 900 / 2100 / 1800 / 1900
 • 4G Network : Hapana
 • OS: Android 7.0 Nougat + XOS 2.2
 • Kioo: 5.0″ HD , 720 x 1280 Pixels
 • Uzito : 145g
 • Graphics Processor : Mali-T720 MP3 450 MHz
 • RAM: 1GB
 • Hifadhi ya Ndani: 16GB
 • Hifadhi ya Nje: Unaweza kuweka memori kadi hadi ya 32GB
 • Kamera ya Nyuma :  8 megapixels, auto focus , dual LED flash
 • Kamera ya Mbele : 2 megapixels na LED flash
 • Bluetooth: v4.0
 • WiFi: Wi-Fi 802.11 b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot
 • Sensors: G-sensor , Light Sensor , Proximity Sensor.
 • Betri: 3060mAh na 250H standby time
SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno Spark Plus K9 bei na Sifa zake

Inakuja Pamoja na :

 • 1 Power Adapter (Charger)
 • 1 USB-Cable
 • 1 User Guide
 • 1 Warranty Card
 • 1 Earphone
 • 1 Film

Smart X5010 ni smartphone maridadi inatengenezwa maalum kwajili ya vijana. Inakuja ikiwa na kioo cha 5.0 inch na screen resolution ya  720 x 1280 Pixels. Ina uzito wa 145g.

Kwa upande wa vifaa vingine, Smart X510 inaendeshwa na Quad-Core MediaTek MT6580 processor inayofanya kazi kwa kasi ya 1.3Ghz. Ina 1GB RAM ili kukuwezesha kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja ndani ya simu yako pia ina 16GB ya hifadhi ya ndani (ROM internal storage) , na unaweza kutumia memori kadi hadi ya 32GB.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kutambua betri na simu ya Tecno kama ni fake au origino

Smart X5010 inatumia mtandao wa 2G & 3G haina uwezo wa 4G LTE. Simu janja hii inafanya kazi kwenye toleo la Android 7.0 Nougat na Infinix X0S v2.2 custom user interface.

Kwa wapenzi wa picha, Infinix Smart X5010 inakuja na 8MP za kamera ya nyuma na 2MP kwajili ya kamera ya selfie. Inaweza kuwa sio simu yenye kamera nzuri ila ni sawa ukilinganisha na bei yake.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako