Sambaza:

Infinix Note 4 (a.k.a. Infinix X572) ni toleo maarufu zaidi la simu za Infinix kwa mwaka 2017. Bei ya Infinix Note 4 kwa Tanzania inaanzia Tsh 380,000. Simu ya mwaka 2016 Infinix Note 3 ilikuwa na kioo cha inchi 6, wakati huu Infinix imekuja na mwonekano bora zaidi wa kioo cha 5.7-inch. Infinix Note 4 inatumia toleo la Android 7.0 ikiwa na 13 megapixels za kamera ya nyuma na 8 megapixels za kamera ya mbele.

Infinix Note 4

Sifa Muhimu za Infinix Note 4

  • 5.7-inch IPS Display, 1080 x 1920 pixels (386ppi)
  • 1.3GHz octa-core MediaTek Helio X10 MT6753 CPU with 2GB/3GB RAM
  • Android 7.0 (Nougat)
  • 16GB / 32GB Storage with support for memory card up to 128GB
  • 13MP Rear Camera and 8MP Front Camera
  • 4G LTE Data
  • Fingerprint Sensor (Front)
  • 4300 mAh Battery with Fast Charging
SOMA NA HII:  Uchambuzi wa simu ya Infinix Hot S X521 na Bei yake nchini Tanzania

Infinix Note 4

Muonekano, Kioo, kamera

Infinix Note 4 ina muonekano mzuri kitu kitakachofanya ujivunie kuwa nayo. Simu hii ya mkononi  inapatikana katika rangi mbalimbalia. Ina kioo cha  5.7-inch IPS na resolution ya 1080 x 1920 pixels.

Kmaera ya mbele imeboreshwa kutoka 5 megapixels hadi 8 megapixels. Hii inakuhakikishia kupiga selfie zenye ubora.

Infinix Note 4 ina kamera ya 13 megapixelsambayo ni sawa na kamera ya Note 3, pia ina mfumo wa dual-LED flash na phase detection autofocus.

Vifaa na Programu

Infinix Note 4  inawezeshwa na  Mediatek MT6753 chipset  ambayo ni 1.3GHz octa-core processor. Pia ina 2GB RAM au 3GB RAM pamoja 16GB au 32GB ya uhifadhi wa ndani na unaweza kuweka memori kadi hadi ya 128GB. Pia kuna Infinix Note 4 Pro ambayo ina 3GB RAM na hifadhi ya ndani ya 32GB. Infinix Note 4 inatumia toleo la Android 7.0 (Nougat) ikiwa na Infinix XOS 2.2 U.

SOMA NA HII:  Bei mpya za simu za tecno nchini Tanzania

Infinix Note 4  ina betri yenye ujazo wa 4300 mAh, ambayo ni ndogo kuliko betri ya 4500 mAh iliyopo kwenye simu ya  Note 3.

Infinix Note 4 pia ina vitu vingine kama Bluetooth 4.2, micro USB, dual-band Wi-Fi, na 4G LTE. Inategemea na eneo ulilopo, uwezo wa LTE bands unatofautiana.

 

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako