Sambaza:

Ni rahisi kusema kwamba Infinix Hot 5 Lite ni toleo la chini la simu yenye gharama nafuu ya Hot 5, kama ilivyoonyeshwa na ‘Lite’ moniker. Infinix Hot 5 Lite ina sifa nyingi zinazofanana na ndugu yake, lakini haina fingerprint scanner na inakuja na RAM ndogo.

Infinix Hot 5 Lite

Sifa Muhimu za Infinix Hot 5 Lite

  • 5.5-inch Touch Display, 720 x 1280 pixels (267ppi
  • 1.3GHz quad-core MediaTek MT6
  • 580 CPU with 1GB RAMAndroid 7.0 (Nougat), XOS 2.216GB
  • Storage with support for memory card up to 32GB
  • 8MP Rear Cam
  • era and 5MP Front Camera3G and Wi-F
  • i4000 mAh Battery with Fast Charging
SOMA NA HII:  Simu 9 Bora za Tecno unazoweza kununua 2017 - Uwezo na Bei

Ubunifu na Kioo

Mtu anaweza kuwa sahihi kusema kwamba hakuna jambo la ajabu kuhusu muonekano wa Infinix Hot 5 Lite. Lakini ina muonekano mzuri .

Bado kuna kioo cha inchi 5.5. Hii inazidi kuwa kawaida siku hizi. Simu ya mkononi  hii ina kioo chenye pixels 720 x 1280.

Kamera na Uhifadhi

Kwa upande wa kamera hakuna kilichobadilika kutoka kwenye Infinix Hot 5. Kuna kamera ya megapixel 8 upande wa nyuma na kamera ya mbele yenye megapixel 5. Zote zinaweza kupiga picha nzuri kutokana na msaada wa LED flash.

Kama ndugu yake, Infinix Hot 5 Lite inakuja na uwezo wa hifadhi ya ndani wa 16GB. Unaweza kuongeza uhifadhi kwa kuweka microSD card.

SOMA NA HII:  Tecno Phantom 5 vs Huawei P8 Lite, Ipi ni Simu kali ?

Uwezo na OS

Simu ya Infinix Hot 5 Lite inatumia MediaTek quad-core processor kama Hot 5.Utofauti wa uwezo wa kufanya kazi unakuja kwenye RAM. Hot 5 Lite ina 1 GB tu,ukilinganisha na 2 GB kwenye simu ya Hot 5. Inafanya kazi kwenye mfumo binafsi wa Infinix XOS 2.2, ambao ni maboresho ya Android 7.0 Nougat.

Sifa Zingine

Unapata betri yenye uweoz wa 4,000mAh kwa uwezo huu unaweza kutumia simu hii masaa mengi bila kuchaji pia ina teknolojia ya kuchaji kwa haraka.

Lakini haina fingerprint scanner kama simu ya Hot 5. Kama simu nyingine, Infinix Hot 5 Lite haina uwezo wa 4G LTE. Inatumia mtandao wa 3G pia ina uwezo wa kawaida wa wireless connectivity, kama Bluetooth na Wi-Fi.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno W3 bei na Sifa zake

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako