Sambaza:

Huawei Nova 2S ni simu janja yenye nguvu ambayo vijana wengi na wapenzi wa picha wataipenda. Ina mpangilio wa kushangaza wa kamera, kioo kikubwa cha HD, vifaa vilivyo na ubora na ubora wa sauti .

Huawei Nova 2S

Sifa na Uwezo wa Huawei Nova 2s

  • 6.0-inch IPS Display, 1080 x 2160 pixels (402 ppi)
  • Octa-core HiSilicon Kirin 960 CPU with 4GB / 6GB RAM
  • Android 8.0 (Oreo), EMUI 8.0
  • 64GB / 128GB built-in Storage, up to 256GB microSD card
  • 16MP + 20MP Dual Rear Camera and 20MP + 2MP Dual Front Camera
  • 4G LTE Data
  • Fingerprint Scanner (Front)
  • 3340 mAh Li-ion Battery

Ubunifu & Kioo

Ina umbo la metali, sitakushangaa ukisema Huawei Nova 2S ina muonekana mzuri sana. Inakaa vizuri kwenye mikono kutokana na kutokuwa na umbo kubwa sana. Huawei Nova 2S ina kioo cha LTPS IPS chenye inchi 6 na resolution ya pixels 1,080 x 1,920.

SOMA NA HII:  Simu Bora Zenye Kamera Nzuri Mwaka 2018

Kamera

Kitu kinachoibeba simu hii ya Huawei Nova 2S ni uwezo na ubora wa kamera zake. Inakuja na jumla ya kamera nne!

Huawei Nova 2S upande wa nyuma ina kamera ya 16MP na 20MP, zote zikiwa na f/1.8 aperture. Pia ina kamera nyingine mbili upande wa mbele zikiwa na 20MP na 2MP kwajili ya selfies . Kamera zake zinapiga picha nzuri hata kwenye mwanga mdogo.

Kamera ya nyuma inajumuisha autofocus na uwezo wa kurekodi video kamili ya HD. Kamera zote mbele na nyuma zinafurahia  msaada wa LED flash.

Vifaa na Programu

Huawei Nova 2S inatumia prosesa ya octa-core HiSilicon Kirin 960 SoC. Processor inapata msaada kutoka kwenye RAM ya  4GB au 6GB RAM, kulingana na toleo unalonunua.

SOMA NA HII:  Mambo 6 ya Muhimu Kuzingati Kabla ya Kununua Simu Mpya

Unapata 32GB, 64GB au 128GB ya uhifadhi. Hii inatosha kwa mahitaji ya watumiaji wengi. Kwenye simu hii ya Android, ambayo inatumia toleo lililoboreshwa la Android 8.0 Oreo, pia unaweza kuweka memori kadi ili kuongeza uhifadhi.

Sifa Nyingine na Uwezo

Huawei Nova 2S ina betri ya 3,340mAh Li-Po. Huawei wanasema tarajia maisha marefu ya betri, kwa kuzingatia jinsi mchakato wa processor kutumia nguvu kwa ufanisi..

Ikiwa sauti ni kitu unachikizingatia zaidi, basi hapa utakuwa umepata kitu unachotakiwa kuwa nacho. Ina mfumo mzuri wa 3D stereo, sauti  kama unayoipata katika ukumbi za filamu na mfumo wa sauti wa Huawei Histen ukifanya kazi vizuri.

SOMA NA HII:  Wanafunzi wa Primary Tanga kuanza kusoma kwa kutumia Tablet

Chaguzi za Sensor ni pamoja na fingerprint scanner, ambayo kwa namna fulani bado inapewa nafasi ya juu kuongeza usalama.

Bei  na Upatikanaji

Huawei Nova 2S bado haijafika nchini Tanzania, Nigeria, Kenya, na Uganda. Ikianza kupatikana, unaweza kunnua simu janja hii kupitia maduka ya mtandaoni hapa nchini. Bei ya Huawei Nova 2S Kwa Tanzania itakuwa kati ya  700000 na Tsh 1400000 kutokana na eneo ulilopo.

 

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako