Simu za Mkononi

Simu Ya Gionee S10 Inamwonekano Wa iPhone Lakini Ina Kamera Nne

Kama unapenda teknolojia,na bado hujaiona iPhone 7 Plus, basi unastahili:

Gionee wametangaza simu mpya na kama ilivyo huenda isifike kwenye soko la hapa nyumbani, ila kuna sababu za kuitazama kwa makini ; Simu hii ina kamera nne!

Jambo la kwanza, jina lake linatamkwa hivi jo-nee, ndio, kama Johnny wa kwenye wimbo wa Yemi Alade.

Pamoja na kuonekana kama iPhone 7 , ikiwa ni pamoja na mistari ya antenna, Gionee wanadai kwamba simu yao mpya S10 ni bidhaa yenye ubunifu mkubwa. Hebu mimi na wewe tuwe mahakimu katika hili.

Inakupa 16 MP na 8 MP camera kwenye Kamera za nyuma na pia ina 20 MP camera na 8 MP camera kwa upande wa mbele.

Vitu vingine vinavyopatikana kwenye simu hii ni pamoja na:

OS: Android 7.0 Nougat, Amigo OS 4.0
Processor: Mediatek MT6757T Helio P25
Display: 5.5-inch, 1080 x 1920 pixel resolution, 2.5D Screen Glass
Dimensions: 155 x 76.8 x 7.4 mm
Weight: 178g
Battery: 3450mAh (non-removable)
RAM:4GB RAM
Storage: 64GB (expandable)
Cam: Dual 16 MP + 8 MP (rear)
Cam: Dual 20 MP + 8 MP (front)
Connectivity: WiFi, Bluetooth 4.0, 4G LTE
Others: Fingerprint, microUSB 2.0, Dual SIM

Sasa, Kamera nne zina matumizi gani. Unauliza:

Gionee wanasema kamera za nyuma zina “af / 1.8 aperture”, inakusaidia kupiga picha nzuri kwenye mwanga mdogo, pia inasaidia kuimarisha utambuzi wa background na kuwawezesha kupata “Taswira ya mkondo (Portrait Mode)” kuliko unayoipata kwenye iPhone 7 Plus. Mbali na hilo zina uwezo wa kupata madhara nzuri za 3D . Wakati kamera za mbele husaidia kupata  “welfie effect”.

SOMA NA HII:  Unamiliki simu ya iPhone ? Apple inapunguza kasi ya simu yako

Mimi sijui lolote kuhusu wewe, ila naomba kujua, je unaweza kununua simu hii kuona inaleta utofauti gani kwenye soko la simu ?

Kwa sasa bei yake ni $379 (Takribani Shilingi 848000).

Mwisho: Pia ina Gionee S10B (inawezeshwa na Helio P10 processor na 4GB ya RAM).

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako