Habari wadau !! Siku hizi makampuni mengi ya simu yanauza simu zao na bei ya simu hizi mara nyingi huwa ni bei nafuu na zinakuja na ofa mbalimbali.

Mitaani kuna simu mpya za android zinazoitwa Smart 7 !! Ni smartphone za Vodafone zinazouzwa na kampuni ya Vodacom kwa bei ya Tsh.70,000/= tu.
Zinatumia mtandao wa 3G, zina memori ya 4GB, kamera ya nyuma ya 2.0MP na RAM ya 512MB. Simu inakuja ikiwa tayari imeunganishwa na intaneti ambapo mitandao kama Facebook, Twitter, WhatsApp, Snapchat na Instagram tayari imeingizwa kwenye simu.
Kwa lengo la kupata ufafanuzi zaidi na kuwapa taarifa watu wengine wanaotaka kununua simu hii, kama umeshawahi kuitumia basi tufahamishe juu ya ubora wake! kuanzia kamera, ufanyaji kazi wa Apps, nk.
Tuambie kama simu za Smart 7 zinazouzwa na Vodacom ni simu nzuri au mbaya.
7 Comments
wakuu nimeipenda sehemu yenu ya kutoa maoni
Hiyo pesa bora ufanyie vitu vingine ama endelea kuikusanya ukanunue simu kali
Yani RAM haijafika hata 1gb hiyo simu itakuwa nzito sana
Kama una matumizi ya kawaida ni nzuri ila kama wewe ni mpenzi wa vitu vikali achana na huo mpango wa kununua simu hii
Inatumia Adroid ipi wadau?
Duuh ukiona kitu kina bei nafuu ogopa sana
Kizuri chajiuza kibaya chajitangaza