Ifahamu Simu Mpya ya Xiaomi Inayofanana Kamera na iPhone X


Huwezi kuzungumza juu ya simu zenye skrini inayofunika sehemu yote ya mbele na kusahau kwamba Xiaomi ilikuwa kampuni ya kwanza dunia kuja na kifaa kama hicho mwishoni mwa mwezi wa Oktoba 2016, kipindi ambacho uvumi kuhusu simu ya iPhone X ulianza kuibuka. Hiyo ndivyo ilivyokuja na simu ya Mi Mix 2, na sasa Mi Mix 2S, iliyozinduliwa hivi karibuni nchini China.

Tofauti na simu za Android nyingi za 2018 zinazotoka China, simu hii hawajainga simu ya iPhone X. Badala yake, bado ina muundo uliozoeleka wa simu za Xiaomi, na inajumuisha kamera ya selfie. Kamera ya nyuma, kwa kiasi fulani, ni clone ya kamera ya iPhone X.

Baada ya kusema hayo, Mi Mix Mix 2 inaonekana kuwa Android flagship ya kweli kwa mwaka 2018. Ni simu iliyotengenezwa kwa  aluminum na ceramic .Inakuja na Qualcomm’s Snapdragon 845, pamoja na 6GB / 8GB ya RAM, na 64GB / 128GB / 256GB ya uhifadhi wa ndani.

Kamera za simu hii zinaonekana kama zinafanana na mfumo wa kamera ya iPhone X. Lakini Xiaomi anasema simu hii ina uwezo wa kutoa uzoefu mkubwa zaidi. Kamera yake ina Sony IMX363 flagship sensor na 1.4μm pixels kwa picha bora zaidi katika mwanga mdogo na teknolojia ya Dual Pixel kwa ajili ya autofocus ya haraka.

Mi MIX 2S pia inakuja na vipengele vya kuunganishwa vya AI, ikiwa ni pamoja na AI voice assistant ili kudhibiti simu janja. Pia ina RAM ya 8GB na ROM ya 256GB, Mi MIX 2S inatoa uwezo kamili wa Qualcomm® Snapdragon ™ 845 ya hivi karibuni kwa utendaji bora zaidi.

Jambo la kuvutia zaidi ni kwamba Xiaomi iliamua kuzindua flagship yake mpya siku ile ile ambayo Huawei, moja ya wapinzani wake wakuu, imezindua matoleo ya Huawei P20 huko Paris, Ufaransa.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA