Simu za Mkononi

Simu mpya ya Huawei P9 Lite Mini. Sifa na Bei yake kwa Tanzania

Huawei P9 Lite Mini ni simu ndogo kwenye familia ya P9 Lite. Ni simu inayofaa kwa watu wanaotaka kununua simu nzuri lakini wana kiwango kidogo cha fedha ikiwa na vipengele kama vile prosesa ya quad-core Qualcomm na RAM ya 2GB.

Uwezo na Sifa za Huawei P9 Lite Mini

  • Kioo:  5.0-inch IPS, 720 x 1280 pixels (294 ppi)
  • Prosesa: 1.4GHz Quad-core Qualcomm Snapdragon 425 CPU with 2GB RAM
  • Mfumo endeshi: Android 7.0 (Nougat), EMUI 5.1
  • Uhifadhi: Ujazo wa ndani (Storage) 16GB, pia unaweza kuweka memori hadi 128GB
  • Kamera: Kamera ya nyuma (Rear) 13MP na Kamera ya mbele (Selfie) 5MP
  • 4G LTE Data
  • Fingerprint Scanner
  • Betri: 3020 mAh Li-ion Battery

Muundo na skrini

Hii inafaa ikiwa unahitaji smartphone unayoweza kutumia kwa urahisi kwa mkono mmoja. Huawei P9 Lite Mini ina upana wa 8mm na uzito wa gramu 145.

Huawei P9 Lite Mini haina skrini ya inchi 5.2 kama ya P9 Lite, badala yake ina skrini ya inchi 5 IPS LCD.  Resolution yake ni 1,280 x 720, lakini hii ni nzuri kwa ukubwa wake.

Kamera na Uhifadhi

Huawei P9 Lite Mini ina kamera ya msingi ya 13MP yenye autofocus na LED flash. Inachukua video 1080p kwenye fps 30. Kwa upande wa kamera ya selfies, unapata safu ya chini (lower resolution) ya 5MP sensor, ikilinganishwa na 8MP ya kwenye P9 Lite.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno Phantom 6 Plus bei na Sifa zake

Hifadhi ya ndani ni 16GB. Pia kuna sehemu ya memori kadi ambapo unaweza kuweka memori hadi ya128 GB.

Utendaji na OS

Huawei P9 Lite Mini ina processor ya qualcomm Snapdragon 425 ambayo kasi yake ni 1.4 GHz. Msaada unatoka kwenye RAM ya 2GB na Adreno 308 GPU.

Usanidi huu utafurahisha watumiaji wa kawaida zaidi. Kifaa hiki kinaendeshwa na programu ya Android 7.0 Nougat.

Sifa nyingine na Uwezo

Kampuni hii ya simu kutoka China imetoa P9 Lite Mini ikiwa na betri ya ujazo wa 3,020mAh Li-Ion ambayo inaweza kukaa siku mbili ukiwa unasikiliza muziki. Ikiwa unahitaji simu yenye fingerprint scanner, basi utaikuta nyuma ya simu hii.

Simu hii inafanya kazi kwenye mtandao wa haraka wa LTE. Vipengele vingine vya kuunganishwa ni pamoja na hujumuisha microUSB 2.0, Bluetooth 4.1 LE na Wi-Fi 802.11 b / g / n na Wi-Fi Direct na Hotspot. Kwa urambazaji, Huawei P9 Lite Mini ina uwezo wa GPS na A-GPS na GLONASS.

Bei na Upatikanaji

Huawei P9 Lite Mini bado haipatikani Tanzania, Kenya, na Uganda. Kwa sasa hatuna data juu ya bei na upatikanaji wake Tanzania, Kenya, na Uganda. Itakapoanza kupatikana, bei ya Huawei P9 Lite Mini nchini Tanzania inatarajiwa kuwa kati ya Tsh 340000 na Tsh 700000 kulingana na eneo lako.

SOMA NA HII:  Unatumia "Lock ? " ya aina gani kwenye simu yako?

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako