Sambaza:

Kila mtu anaanza mwaka na mipango yake, 2016 ndio hii na bado tupo tarehe za mwanzo za mwezi januari, kama ishu ya kubadili simu iko kwenye mipango yako ya mwanzo wa mwaka basi naomba nikufahamishe machache kuhusu hii Phantom 5.

Kwa sababu Tecno wamethibitisha kuwasogezea Watanzania matoleo kadhaa ya simu za smartphones zenye viwango vyake sokoni, basi kuna hii mpya ambayo iko sokoni kwa sasa mtu wangu !!

Tecno wamenithibitishia kwamba Phantom 5 ina uwezo mkubwa wa kuhifadhi kumbukumbu pamoja na memory card kubwa, processor, pamoja na RAM ya GB 3.. kingine ni usalama wa kutosha pia kwa sababu ina Fingerprint Identification Sensor ambayo ni alama za vidole vyako tu zitaifungua simu yako na uitumie, sio mtu mwingine.

SOMA NA HII:  Njia bora ya kuroot simu yoyote ya tecno bila kutumia kompyuta

Usihofu kuhusu chaji mtu wangu, betri yake inaweza kudumu kwa muda mrefu hiyo… ishu za umeme wa mgao hutakuwa na hofu kukosekana hewani, camera zenye flashlight upande wa nyuma na mbele…. naambiwa pia kwamba mzigo uko nchi nzima kwenye maduka ya simu na mawakala wa Tecno, hakika hii sio ya kuiachia.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako